Saturday, August 20, 2011

Matema Beach

Leo nimeshinda Matema Beach, kandoni mwa Ziwa Nyasa. Hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika mahali hapa. Niliweka kipaumbele kufika hapa katika safari ya kuzunguka na wanafunzi kutoka Marekani ambao nimewaleta Tanzania.




Matema Beach panapendeza sana. Ingawa ni kijiji kidogo, kuna hoteli kadhaa hapa. Moja ni Lutheran Center ambayo inaonekana pichani kushoto.





Hapa ni baadhi ya nyumba za kulala wageni hapo Lutheran Center.


Hapa kushoto ni kibanda kimojawapo cha kulala wageni hapo Lutheran Center.











Hoteli nyingine ni Matema Beach Resort. Hapo kushoto kuna picha za baadhi ya nyumba za kulala wageni.








Ninapokuwa maeneo kama haya ya Matema Beach, najikuta nikitafakari hili na lile. Wakati huu ufukwe wa Matema Beach ni huru kwa wananchi kutembea, kuogelea, na kupumzika.

Lakini nahisi kuwa siku itakuja ambapo wenye pesa watajichukulia sehemu hizi na kujenga uwigo hadi ziwani. Baada ya kuwekewa uzio, wananchi hawataweza kupita tena maeneo hayo. Hali hii nimeiona sehemu mbali mbali Tanzania, kama vile Ukerewe. Huu ni ubovu wa sera za serikali ya Tanzania ambao unanikera.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Duh! umeniwahi kuweka hizi picha maana nami nilikuwa hapo...Ahsante.

Mbele said...

Shukrani kwa ujumbe. Sikujua kuwa umefika mahali hapa. Ni pazuri sana, nami nilipiga picha nyingi ambazo nategemea kuzitumia katika blogu zangu.

Yasinta Ngonyani said...

Nilifika na kweli ni ppazuri sana. Nilipapenda mno. Nami pia niana picha kadhaa ntazimwaga karibuni pia.

Anonymous said...

profesa mbele siku moja wapeleke wanafunzi wako pori la minziro kule kyaka kagera wakaone nyoka mwenye miaka 280

Mbele said...

Anonymous, shukrani kwa hizi taarifa za nyoka huyu wa ajabu. Ni mambo ya kufuatilia siku za usoni. Kila la heri.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...