Wednesday, October 12, 2011

Maktaba ya Mkoa, Ruvuma

Nilipiga picha hii ya maktaba ya Mkoa, Ruvuma, tarehe 30 Julai mwaka huu. Niliwahi kuingia katika maktaba hii, ambayo iko mjini Songea, miaka kadhaa iliyopita, lakini safari hii sikupata muda. Nilizunguka maeneo mengine, kama vile Makumbusho ya Maji Maji, ambayo habari zake nategemea kuziandika baadaye.

Napenda kuandika habari za maktaba za Tanzania. Nimeshaandika kuhusu maktaba ya Lushoto, Kilimanjaro, na Iringa. Nitaendelea kufanya hivyo.

5 comments:

Simon Kitururu said...

nimatumaini yangu kuna vitabu humo na vitabu vyenyewe wasomao sio wadudu MENDE au MCHWA kwa kuvimegua!:-(

Mbele said...

Mimi pia, nilipokuwa naandika habari hii, niliwazia kuongelea suala la usomaji. Nilitaka kuuliza ni watu wangapi wanaoishi Songea wanafahamu ilipo maktaba hii na wana mazoea ya kuingia na kusoma.

Suali hili sherti liulizwe kwa wale wanaoishi katika miji mingine ambayo ina maktaba, kama vile Arusha, Tanga, Dar es Salaam, na hata kwangu Mbinga. Je watu wa miji yetu wanajua maktaba ilipo?

Mwalimu Nyerere alijitahidi kuweka maktaba nyingi nchini. Lakini tangu aondoke, wa-Tanzania tumeamua kuwa kinachohitajika kwa maslahi ya Taifa letu si maktaba bali baa na kitimoto :-)

Simon Kitururu said...

:-(

Na nisikitikaye ni muhudhuriaji pia wa mpaka huko baa na kitimoto kwangu si haramu!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Ngoja niwe mkweli sijawahi kwa kweli kuiona hiyo maktaba na sijui ipo wapi au labda pale karibu na jimbo kuu?

Mbele said...

Dada Yasinta umenichekesha sana leo. Yaani sina mbavu, ila wanasema msema kweli ni kipenzi cha Mungu :-)

Maktaba iko mtaa ule ule wa Jimboni, unaotokea kituo kikuu cha mabasi. Unapita Jimboni, duka la vitabu la Kanisa Katoliki, soko kuu, benki pale kushoto, kanisa la zamani pale kulia, halafu juu kidogo tu, upande huo huo wa kulia ndipo ilipo maktaba hiyo, kabla kabisa ya kufika Bomani.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...