
Hapa kushoto niko na Mwalimu Dallagrana nyumbani mwake mjini Madison, Wisconsin. Yeye ndiye alinialika Madison wiki iliyopita, kuongea na wanafunzi wake kuhusu kitabu cha
Africans and Americans.
Mwalimu Dallagrana aliishi Lesotho miaka ya mwishoni ya sabini na kitu, akijitolea katika programu ya
Peace Corps. Tulifahamiana nilipojiunga na Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison mwaka 1980 kwa masomo ya juu.

Miezi michache iliyopita, Mwalimu Dallagrana alikinunua na kukisoma kitabu hicho, akaona kinafaa kwa wanafunzi wake. Ndipo alipowapa sehemu kadha wa kadha za kitabu hiki wasome, na hatimaye akanialika kwenda kuongea nao, kama nilivyoelezea
hapa.
Hapa kushoto naonekana nikisaini kitabu hicho na hapo mbele kabisa ni kitabu changu kingine,
Matengo Folktales, ambacho nilisaini pia.
No comments:
Post a Comment