Tuesday, October 4, 2011

Taswira Tata Kutoka Igunga

Picha hii hapa kushoto, ya DC wa Igunga na watu wanaosemekana ni wafuasi wa CHADEMA imezua zogo kubwa miongoni mwa wa-Tanzania wakati wa kampeni Igunga. Haijawa rahisi kwangu kujua kiini cha tukio hili wala ukweli wake kikamilifu. Kwa hivyo, sikutoa tamko lolote, ingawa naona purukushani baina ya hao wanaume na huyu mama.


Hapa kushoto kuna picha ya tukio jingine lililotokea Igunga baadaye katika mazingira haya haya ya uchaguzi. Taarifa zinasema kuwa huyu mama ni mwanachama wa CHADEMA, na hapo anasukumizwa garini na askari wa kiume. Labda wale waliotoa matamko kuhusu lile tukio la mwanzo wana lolote la kusema kuhusu tukio hili la pili. (Chanzo Kapingaz)

Ili kuepusha dhana na hisia zisizo na ukweli, napenda kusema kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Sioni kama ujenzi wa demokrasia au kuwepo kwa demokrasia katika mazingira yetu kunahitaji chama au vyama. Nimeelezea mtazamo wangu huo katika kitabu cha CHANGAMOTO.

3 comments:

tz biashara said...

Mimi kama mtanzania sijaona bado kiongozi au viongozi ambao tunaowahitaji.Tunawahitaji viongozi walio na busara,amani,upendo,utaifa,bidii,wenye kuwaunganisha watanzania,kikidhi haja za watanznia,mkweli,msimamo,kujali,mleta maendeleo na mfanya kazi kwa bidii.
Watanzania tunahitaji kuepukana na viongozi walio walafi,wasiojali wananchi,wanafik,wavivu,wenyekujali maslahi yao,wadini,mafisadi,porojo za uongo,vurugu,wanao watenga watanzania, na wasio na maarifa ya kuokoa nchi.Mengine mtanisaidia.
Kwa kweli bado sijaona chama kitakacholeta mabadiliko ktk nchi.Lakini vilevile profesa ninaamini wananchi pia wanahitaji kubadilika sio kwa viongozi tu.Wananchi maisha wanayoishi ni ya kubahatisha yasio na mpangilio.Tuache uvivu na uchafu pamoja na kuendekeza starehe kuliko kutafuta elimu.Sisi wenyewe ni wachafu wa mazingira kwa kujua serikali ndio kazi yao ya usafi.

tz biashara said...

Hayo yaliyotokea huko Igunga kuhusu huyo mama ni jambo la kusikitisha japo mwanzo wake siujui.Nasio lazima awe muisilamu hata akiwa ni dini yoyote ile.Hakuna mtu yoyote ana haki ya kumvua mwananmke au mwanamme kwa kivazi chochote alichokivaa.Nasio ktk mavazi tu ila walimpiga inavosemekana na sio jambo la kulifurahia na hata viongozi wa Chadema walitakiwa waombe radhi kwa huyo mama.Lakini kutokana na chuki zinavozidi kushamiri za udini na siasa uchwara ndio unatufanya kuishi kihunihuni bila heshima.
Na hao askari hiyo ni kawaida yao kudhalilisha watu siku zote sio kwa CHADEMA tu bali ni kwamnyonge yoyote.Democracia hapa haijafika bado ila tunaishi kiubabebabe tu na kutafuta mlo mara tatu.
Watanzania leo wanafikiri demokrasia ni kuwa na waimbaji wengi na mastaa wa muvi ambazo zinafundisha ngono pamoja na VODA COM kuwadhalilisha dada zetu na kuwaweka nusu watupu huku watu wakishangilia na kinywaji kinaendelea.
Kwakweli tupo nyuma sana tuombe mungu ili azaliwe kiongozi mpya atakaye leta maendeleo kuitoa nchi ktk umasikini.

Simon Kitururu said...

Mmmmmh!

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...