Tarehe 9 Februari 2019, niliendesha warsha kuhusu "Culture and Globalization." Tulifanyia Lion Hotel, Sinza, Dar es Saalam. Washiriki tulikuwa wachache, lakini tuliongelea na kueleweshana mambo mengi. Tulianza kwa kujitambulisha, kila mtu na shughuli zake. Kisha nilitoa maelezo kuhusu dhana ya "globalization," nikifuatilia historia na aina za "globalization." Halafu nilielezea jinsi tofauti za tamaduni zinavyohusika katika "globalization," na athari zake hasa katika hizi zama zetu na zijazo. Baada ya maelezo yangu, washiriki wa warsha tulijumuika na kutoa mifano ya athari hizo. Washiriki wa warsha walipata fursa ya kununua nakala za Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, ambacho ni msingi mojawapo wa mada ya warsha. Kitabu hiki kinapatikana katika duka la vitabu la A Novel Idea, lililopo Slipway, Msasani, na pia duka la Kimahamana Literature Center, Arusha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment