Watanzania jitokezeni kwenye mijadala ya elimu

Habari hii imechapishwa katika gazeti la Habari Leo

Imeandikwa na Na Simon Nyalobi; Tarehe: 7th November 2009

WATANZANIA wametakiwa kujenga tabia ya kuandika machapisho ya utafiti wao na kujitokeza katika mijadala ya kimataifa kuhusu elimu badala ya kuogopa na kukaa pembeni.

Mwito huo ulitolewa jana Dar es Salaam na Ofisa Mipango ya Elimu wa Shirika la Oxfam tawi la Tanzania, Mary Soko wakati wa akifunga warsha ya siku tatu ya Jumuiya ya Utendaji wa Elimu nchini iliyokuwa na washiriki 40 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Soko alisema kuwa Wataznania wengi hawajitokezi katika makongamano ya kimataifa kuonesha utafiti wao ikilinganishwa na mataifa mengine hususani Nigeria ambayo raia wake hujitokeza kila kongamano la usomaji wa vitabu linapotokea.

Alisema kuwa hata makongamano yanayofanyika hapa nchini, hayana muamko kwa kuwa watanzania wengi wamekuwa nyuma kushiriki. Kutokana na hali hiyo, amewataka sasa kujitokeza kila yanapotokea makongamano ya usomaji wa vitabu ili kuiweka nchi katika ramani ya wasomi kwani uwezo wa kufanya hivyo wanao.

Hata hivyo aliasa tabia ya kusoma iboreshwe katika jamii hususani wadau wa elimu, ili waongeze maarifa ya kuandika utafiti wao kwa usahihi.

Pia aliwataka walimu kuacha kulala na badala yake waihamasishe serikali kuhusu mustakabali wa elimu ili kudumisha kiwango cha elimu nchini kwani wakishindwa wao taifa nalo litashindwa.

Katika hatua nyingine alilitaka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Taasisi ya Ukuzaji wa Mitaala na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushirikiana kwa pamoja ili kuboresha kiwango cha elimu nchini.

Comments

Simon Kitururu said…
Inahitaji kujiamini sana kujitokeza kwenye mijadala ya elimu wakati unawasiwasi na elimu yako.

Swali:

Elimu Tanzania sasa hivi unafikiri inaweza kukufanya ujiamini kubishana na Mchina kielimu au hata kujiamini na jibu lako kielimu wakati unabishiwa na Mkenya kuwa kwanini inafikiriwa na wengi wasio wajanja Mlima Kilimanjaro uko Kenya?

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini