Thursday, September 17, 2009

Warsha: "Utamaduni, Utandawazi na Maendeleo," (Tanga, Agosti 29)


Tarehe 29 Agosti niliendesha warsha Tanga, Tanzania, mada ikiwa ni "Utamaduni, Utandawazi na Maendeleo". Warsha hii ilifanyika katika kituo kiitwacho Meeting Point Tanga na ilidumu kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Hapo juu anaonekana Mama Ruth Nesje, mkurugenzi wa kituo, akinitambulisha kwa washiriki wa warsha.

Niliamua kufanya warsha hii kutokana na uzoefu wangu wa kuelezea masuala haya ya utamaduni kwenye vyuo, taasisi, makampuni, makanisa, jumuia mbali mbali na watu binafsi huko Marekani. Warsha hii ilikuwa na mvuto mkubwa kwa washiriki na iliamuliwa kuwa zifanyike warsha hizi siku zijazo. Kitu kimoja kilicholeta msisimko na mjadala mkubwa ni makala yangu "Maendeleo ni Nini?"

Ninapangia kuandika zaidi kuhusu warsha hii, na nyingine ambayo niliendesha Dar es Salaam tarehe 5 Septemba, ila nimeona niweke hii taarifa fupi hapa, kwa sasa. Kama kianzio, nimeweka picha chache zilizopigwa siku hiyo.




(Photos by Vesla Eriksen)

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kazi nzuru Prof. Na asante kwa kutukumbuka kwa kuweka habari hii na picha hapa kibarazani kwako nasi tumefaidi au labda niseme (mimi).

Mbele said...

Dada Yasinta, shukrani. Kadiri siku zinavyoenda, na Mungu akipenda, nitakuwa naendesha hizi warsha sehemu mbali mbali Tanzania. Ujumbe wangu ni kama wanavyosema vijiweni: kaeni mkao wa kula :-)

Simon Kitururu said...

Sie tusha kaa mkao wa kula na tunakusubiri Prof.:-)

Nami nirudie alichosema Dada Yasinta, ASANTE kwa kutumegea habari hii na tuna subiri zaidi kuhusu kilichojiri huko Tanga !

Mbele said...

Leo nimeweka taarifa kwenye blogu hii kuhusu warsha niliyoendesha Dar es Salaam tarehe 5 Septemba. Bofya hapa. Nadhani nitakachofanya ni kuandika mawazo ya kuunganisha uzoefu wote huo, kwani nimejifunza mengi.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...