Thursday, September 10, 2009

Nimeonana na Mheshimiwa Michuzi


Tarehe 4 Septemba, 2009 ilikuwa siku maalum kwangu, kwani nilipata bahati ya kuonana na gwiji wa blogu, Mheshimiwa Michuzi ofisini kwake pale Mtaa wa Samora, Dar es Salaam. Hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuonana na gwiji huyo.

Tuliongelea mambo mengi yahusuyo blogu na mawasiliano ya kisasa kwa ujumla. Kwa mfano, alikumbushia mkutano wa wanablogu unaopangwa kufanyika Dar es Salaam mwezi Desemba mwaka huu. Nilimwona Michuzi kuwa mtu mwenye hamu ya kuona maendeleo. Hasiti kutoa ushauri wa kuwasaidia wengine. Alisema kuwa anapitia blogu nyingi, na hapo akaniambia kuwa picha iliyopo kwenye blogu yangu si nzuri. Hapo hapo aliniambia nisimame na akanipiga picha nikaiweke kwenye blogu.

Michuzi anaheshimu taaluma yake na anapenda kuona wanablogu wanasukuma mbele gurudumu la mawasiliano hayo kwa kila mmoja kutafuta kipengele maalum na kukiendeleza, iwe ni taaluma, burudani, na kadhalika. Michuzi alisema, kwa mfano, si kila mmoja anaiweza shughuli ya mwanahabari. Tuliongelea mengi, na pia tulifanya mahojiano haya hapa.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Naona ni bahati kubwa kuonana ana kwa ana na mwanablog yeyote yule na hasa kama kaka Michuzi. Hongera Pro.

Sisulu said...

mimi natamani sana kuonana sana na wewe profesa umekuwa mmoja wa wanaonipa hamasa ya kuandika. MUNGU akupe nguvu mimi ni Tandasi ni tembelee katika blog yangu ;ndotoyangu-harakati na nione umefika wasaalam huko ughaibuni.nkosi sikeleli Afrika

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwa nini ukaamua kuonana na michuzi pekee? ili aweze kutangaza ishu ya tng zaidi au?

good

Mbele said...

Ndugu Kamala, uamuzi wa kunikutanisha na Michuzi ulifanywa na jamaa pale Dar ambao wanafahamiana na Michuzi. Kuna mkutano wa wanablogu unaopangwa kufanyika Dar Desemba hii, na nina hakika wanablogu watakaohudhuria watafaidika sana na ushauri wa Michuzi. Anatamani sana tufanikiwe.

Mbele said...

Ndotoyangu, shukrani kwa ujumbe wako. Insh'Allah tutapata fursa ya kuonana.

mandela pallangyo said...

Tena ingefaa michuzi ndo aseme amekutana na mh. MIMI NAONA NI MTU MDOGO SANA KWAKO HUYO.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...