Nashukuru kuwa safari ya Tanzania, mwezi Januari mwaka huu, nikiwa na
wanafunzi 29, ilienda vizuri sana. Wanafunzi kadhaa walinipiga picha
nikiwa kazini.
Hapa ni pembeni mwa Ziwa Manyara. Nawasomea wanafunzi maneno murua kutoka Green Hills of Africa, ambayo yanahusu sehemu hiyo.
Ni pembeni mwa Ziwa Manyara. Nawasomea wanafunzi vifungu kutoka Green Hills of Africa kuhusu sehemu hiyo.
Hapa ni Namanga. Naonekana nikisoma kitabu cha Hemingway, True at First Light, ambacho kilikuwa ni andiko mojawapo muhimu katika kozi yetu.
Hapa ni Karatu, nikiwa na kitabu cha Hemingway, Green Hills of Africa. Ni matayarisho ya kipindi.
Darasa kuhusu Green Hills of Africa limekolea. Ni Karatu hapo.
Darasa kuhusu Green Hills of Africa linaendelea, Karatu.
Hapa ni Babati. Darasa linaendelea.
Hapa niko katika maandalizi ya kipindi, katika Colobus Mountain Lodge, pembeni mwa Arusha National Park.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment