Thursday, February 21, 2013

Maonesho Makubwa St. Paul, Minnesota, Kuhusu Watu Weusi

Tarehe 23 Februari hii, yaani keshokutwa, kutakuwa na maonesho makubwa mjini St. Paul, Minnesota, kuhusu historia, utamaduni, na mambo mengine ya watu weusi, kuanzia wale wa Afrika hadi wale walioko diaspora, yaani sehemu mbali mbali za dunia.

Nitashiriki, kama mwandishi na mwalimu. Nimeshalipia meza na hapo nitaweka machapisho yangu. Nangojea kwa hamu kuongea na watu siku nzima kuhusu masuala ninayoyashughulikia, kama vile utafiti katika mila, desturi, na fasihi; tofauti za tamaduni baina ya wa-Afrika na wa-Marekani, masuala ya kuwapeleka wanafunzi Afrika, faida na changamoto zake.

Kila yanapotokea maonesho ya aina hii, huwa ni fursa ya kukutana na watu wengi na kuelimishana. Nawakaribisha wote watakaopenda kuonana nami. Muhimu zaidi ni kuwa nawahimiza wote wanaoishi maeneo haya ya Minnesota kuhudhuria. Ni fursa nzuri na ya pekee kielimu kwa watu wazima, vijana na watoto.

Kwa taarifa zaidi kuhusu maonesho haya, soma hapa na hapa.

2 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Tunasubiri kwa hamu taarifa hizo (We await with bated breath those great tidings from the tamasha, Prof.)

Mbele said...

Thank you very much, for your encouraging words. I wish you were here; we would have talked a great deal.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...