Mgeni rasmi, aliyetoa hotuba ya ufunguzi wa maonesho, alikuwa Dr. Julianne Malveaux, ambaye ni msomi aliyebobea, hasa katika masuala ya uchumi, na aliwahi kuwa rais wa Chuo cha Bennett.
Hapa vijana wanaopiga ngoma na kucheza. Niliwapiga video kwa dakika kadhaa.
Siku nzima, watu walikuwa wanafika, kwa wakati wao.
Huu ni ukumbi ambamo mambo mengi yalifanyika, kama vile hotuba na maonesho ya mitindo ya mavazi.
Maonesho ya mitindo yanaendelea
Katika shughuli za aina hii, daima nakutana na watu wanaonifahamu, na wengi huwa wamesoma vitabu vyangu. Huyu mama anayeonekana kushoto kabia alipofika kwenye meza yangu, alisisimka ghafla alipoona kitabu cha Africans and Americans, akaanza kuongelea jinsi alivyokinunua miaka mingi iliyopita na jinsi anavyokipenda. Watu waliokuwa hapo kwenye meza yangu walibaki wanamsikiliza, naye akachukua muda kuelezea tulivyokutana. Nilikuwa nimemsahau, lakini kutokana na maelezo yake, nilianza kupata kumbukumbu.
Huyu mama hapa kushoto ni mdau wangu wa kuaminika. Pamoja na kuwa ni msomaji wa maandishi yangu, tumeshiriki mikutano mbali mbali yanayowahusu wa-Afrika na wa-Marekani Weusi. Yeye na mume wake, ambao ni wa-Marekani Weusi, tunafahamiana vizuri sana. Mume wake alipiga hii picha.
2 comments:
Asante sana, Prof, kwa taarifa hizo. Umekuwa macho yetu nasi waBara la-Afrika. Tunafurahi kwa mafanikio hayo.
Asante kwa ujumbe. Ni kweli, najitahidi kutuwakilisha wa-Afrika. Kwa vile mimi ni mwalimu ninayetafiti na kufundisha kuhusu mambo ya Afrika na dunia kwa ujumla, na kwa vile mimi ni mwandishi, shughuli hii ya kuwakilisha hainipi shida, bali naifurahia.
Post a Comment