Nimekuwa kimya kwa karibu mwezi mmoja. Kisa? Nilileta wanafunzi Tanzania, kutoka Chuo cha St. Olaf ambapo nafundisha.
Niliwaleta wanafunzi hao ili kuwafundisha kozi ambayo niliitunga, kumhusu mwandishi maarufu Ernest Hemingway, ambaye alisafiri na kuishi hapa Afrika Mashariki, hasa Kenya na Tanganyika, mwaka 1933-34 na 1953-54.
Tulifika Tanzania tarehe 3 Januari, tukapitia maeneo kadhaa aliyopitia mwandishi huyu hapa nchini petu, tukisoma maandishi yake kuhusu safari zake na matukio mbali mbali sehemu hizo. Maandishi hayo ni riwaya, hadithi fupi, insha, na barua.
Ingawa kazi hii ni nzito, yenye vipengele vingi, nina uzoefu nayo. Nilishaendesha kozi ya aina hii siku zilizopita, kwa wanafunzi wa Chuo cha Colorado, kama nilivyoelezea hapa
Hapo pichani wanaonekana wanafunzi niliowaleta mwaka huu. Ilikuwa ni jioni ya tarehe 28 January, wakati nilipowafikisha uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, tayari kwa safari ya Marekani. Insha Allah nitaweka picha na maelezo mbali mbali katika blogu hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment