Yawezekana kuna wa-Tanzania ambao hawajui kuwa wa-Maasai wanajitahidi kuwapa watoto wao elimu ya shuleni. Hayo nimeyaona katika pita pita zangu sehemu mbali mbali katika nchi ya wa-Maasai.
Yawezekana pia wako ambao watasikitika kuona kuwa shule hii ni ya miti na nyasi, badala ya matofali na bati au vigae. Hilo ni suala la kujadiliwa, kwani ni tata.
Nami niliwahi kusema machache kuhusu suala hili. Niliandika makala kuhusu darasa chini ya mti. Soma hapa.
No comments:
Post a Comment