Sunday, February 17, 2013

Profesa Anapoyaruka Majoka

Katika safari zangu za Tanzania na wanafunzi, huwa najitahidi kwa uwezo wangu wote kuwafundisha vizuri. Papo hapo, najitahidi kuwaburudisha. Ikipatikana fursa ya kuyaruka majoka, ninawajibika vilivyo, na wanafunzi wanabaki hawana mbavu. Mbali ya kwamba burudani ni muhimu katika maisha, napenda kufanya mambo ya aina hii ili kuwaweka wanafunzi sawa kisaikolojia kwa kazi ya kitabu inayowakabili.

Hizo picha zilipigwa Longido, tarehe 27 Januari, siku ya mwisho ya kozi yetu. Mchana wa siku hiyo, wanafunzi walishafanya mtihani wa mwisho, ikabaki sasa kujiburudisha jioni hadi usiku. Palikuwa hapatoshi.

2 comments:

PBF Rungwe Pilot Project said...

Hongera Profesa kwa kuweza kushuka hadi kiwango cha kuruka majoka na wanafunzi wako. Mimi naweza kuita hicho ni kipawa pekee ambacho kiko kwa nadra kwa Maprofesa wengi duniani. Hakika wanafunzi wako wanakuwa huru kwa maana umevunja mipaka ya kiakademia, jambo ambalo naona linatakiwa sana kujengwa hapa petu, ili yumkini Profesa na mwanafunzi wawe na mahusiano mamzuri.

Rachel Siwa said...

Inapendeza sana...

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...