Tuesday, November 9, 2021

WaKenya Wazidi Kukinadi Kitabu


Nimewahi kuandika mtandaoni tena na tena nikiwasifu na kuwashukuru waKenya kwa jinsi walivyokuwa bega kwa bega nami katika utafiti na uandishi wangu.

Huku Marekani, waKenya wamekuwa wasomaji na wapiga debe wangu wakuu kama nilivyotamka, kwa mfano, hapa na hapa.

Sasa amejitokeza mKenya mwingine, Joy Awe, aishiye uJerumani. Yeye ni mwanzilishi na mratibu wa jumuia iitwayo African Women in Europe.

Ameweka picha zake mtandani akiwa na kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, pamoja na ujumbe huu:

Highly recommended book to read especially diaspora or anyone wanting to do business in Africa. Available on Amazon.

Naendelea kuwashukuru waKenya kwa mshikamano nami.

1 comment:

Mbele said...

Leo nimeona taarifa kuwa Joy ameikwaa tuzo ya Global African Awards. Ni heshima kubwa, ambayo baadhi ya watu waliwahi kuipata ni Rais wa Ghana, Mheshimiwa Nana Akufo-Addo, kama inavyoelezwa katika taarifa hii.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...