
Saturday, November 6, 2021
Msomaji Wangu Mpya, mTanzania wa Czech
Katika kufuatilia Facebook, YouTube, na Instagram, nimeona shughuli za Corona, za ufundishaji wa kiSwahili na uandishi wa vitabu vya watoto. Vitabu alivyochapisha ni The Rooster's Voice, Sauti ya Jogoo, na Grandma Pipi and the Roses.
Juzi nilimwandikia kuwa nimeagiza vitabu vyake Amazon, naye hima akaniletea picha akiwa ameshika kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. alichoagiza hivi karibuni mtandaoni.
Mara tu baada ya kukipata kitabu changu, amekisoma na kukiongelea mitandaoni Instagram na Facebook akiwahimiza watu waendao Marekani, Ulaya, na Tanzania wakisome. Amesema pia kuwa ameagiza kitabu changu cha Matengo Folktales. Ni bahati njema kufahamiana na mwalimu na mwandishi mwenzangu, mTanzania aishiye ughaibuni. Tunategemea kubadilishana mawazo na uzoefu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Ukizunguka mitaani Dar es Salaam, utakuta matangazo mengi ya waganga wa kienyeji. Waganga hao wanatoka sehemu mbali mbali, kama vile Sumbaw...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
No comments:
Post a Comment