Wednesday, October 6, 2010

Vitabu Vyangu Kwa Bei Nafuu

Lulu.com, ambako nachapisha vitabu vyangu, kumetokea tangazo linalotoa fursa kwa mwandishi kupunguza bei ya vitabu vyake akipenda.

Kwa heshima ya wasomaji wangu, nimeamua kutumia fursa hiyo. Nimepunguza bei ya vitabu vyangu vyote kwa mwezi huu Oktoba.

Vitabu hivi vimetajwa hapo kulia na pia hapa. Bofya sehemu ya kununulia, ili kuona punguzo hilo.

Wale ambao hawanunui vitu mtandaoni na wanavihitaji vitabu hivi wanaweza kuwasiliana nami kwa barua pepe: info@africonexion.com.

Siku ya mwisho ya punguzo hili ni Oktoba 31.

2 comments:

emuthree said...

Ahsante kwa punguzo hilo. Mimi nashngaa kwanini watu wengi sasa hawapendi kusoma, ila wanpenda kutizama luninga, computer picha? Hawajui kusoma kunaongeza akili ya kufikiri!

Mbele said...

Ndugu emu-three, asante kwa mchango wako. Watanzania wana visingizio elfu inapokuja kwenye suali la kwa nini hawasomi vitabu au kwa nini hawanunui vitabu.

Wengi utawasikia wakidai kuwa m-Tanzania wa kawaida anaishi kijijini ambako hakuna umeme, na atasomaje? Hii ni hoja ya kipuuzi, maana wengi wetu tulikulia vijijini, tukisomea koroboi.

Wengi utawasikia wakidai kuwa kipato cha m-Tanzania wa kawaida ni kidogo sana, kiasi kwamba hata mlo moja kwa siku anapata shida kuumudu. Hii hoja tuliijadili kiasi hapa.

Inapokuja kwenya vitabu kama vyangu, kwa muda mrefu wa-Tanzania wengine walikuwa wananilalamikia kuwa kwa vile naandika ki-Ingereza, nawanyima fursa ya kusoma maandishi yangu. Hii hoja, kama nilivyoelezea katika mahojiano kule Kombolela Show, Oktoba 2, inayumba. Kwa nini wa-Tanzania wasijibidishe kujifunza ki=Ingereza na lugha zingine? Huu ni uvivu.

Pamoja na hayo, mimi nimeshajitosa katika kuandika kwa ki_Swahili pia. Tayari nimechapisha kitabu, CHANGAMOTO ambacho ni mkusanyiko wa insha kuhusu masuala mbali mbali ya jamii yetu, utamaduni, elimu, uchumi, siasa na kadhalika. Sasa nangoja nione kama hao wa-Tanzania watakitafuta na kukisoma kitabu hiki, maana kisingizio cha lugha hakipo hapa.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...