Sunday, February 19, 2012

Mitaani Arusha

Nimefika Arusha mara kadhaa, na nina picha nyingi za mji huo. Kama nilivyofanya kwa miji mingine, kwa mfano Namanga na Mbinga, naleta picha chache. Hapana shaka kuwa baadhi ya wasomaji wa blogu hii hawajafika Arusha. Nataka wapate fununu fulani.








Hapa kushoto ni mtaa wa kati kati ya mji, ambapo pana posta na ofisi za usafiri wa ndege, na hoteli na migahawa. Pana maduka ambamo mtu unaweza kununua vitabu na nguo na kazi za sanaa.









Hapa kushoto ni mnara wa kumbukumbu ya Azimio la Arusha. Azimio la Arusha lilitangazwa hapa Arusha, mwaka 1967.

Mji huu una historia ya kusisimua. Kati ya waasisi wake ni Kenyon Painter, mwekezaji m-Marekani kutoka Ohio. Alijenga posta, kanisa, hospitali, na majengo mengine muhimu, zaidi ya kufungua mashamba ya kahawa na kituo cha utafiti cha Tengeru.
Kwa zaidi ya karne moja, watu wengi maarufu kutoka duniani kote wamefika au kupita Arusha, kuanzia viongozi wa nchi hadi watengeneza filamu na waandishi maarufu kama Ernest Hemingway.





Umaarufu wa Arusha siku hizi uko zaidi kwenye utalii, mahakama ya Rwanda, vyuo na taasisi kama vile ESAMI na Tropical Pesticides Research Institute.











Picha ninazoleta leo zimepigwa katika eneo la katikati ya mji.













Kwa vile nimefika Arusha mara kadhaa, na wanafunzi kutoka Marekani, baadhi ya watu mitaani wananifahamu, kama hao jamaa ninaoonekana katika picha hapa kushoto. Tunafurahi tunapokutana, na michapo inakuwa mingi.










2 comments:

tz biashara said...

Profesa napenda kuona picha za mikoani,lakini naomba nikuulize tafadhali ni swali ambalo huwa linanitatiza.Kwanini watu waliozaliwa na kukulia Arusha meno yao yametofautiana na mikoa mingine.Ila sina uhakika kama Moshi na wenyewe wanamatatizo hayo au mkoa wowote ule.Naomba unitoe ushamba kidogo maana wakati ule mimi mdogo nilikuwa nasikia maji yao ndio yanawafanya meno kubadilika rangi.

Mbele said...

Bahati mbaya sina utaalamu wa somo hilo, ila nakumbuka tulifundishwa kuwa ni suala la kemikali iliyomo ndani ya maji iitwayo "fluoride."

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...