Siku kadhaa zilizopita, niliandika ujumbe wa shukrani kwa mafanikio ya kozi niliyofundisha Tanzania mwezi Januari juu ya mwandishi Ernest Hemingway. Nilikuwa na wanafunzi 29 wa chuo cha St. Olaf. Leo nimepata ujumbe kutoka kwa wazazi wa mwanafunzi mmojawapo, ambao ninauleta hapa. Nimebadili jina la mwanafunzi, na ninamwita Kijana:
Dear Professor Mbele --
We want to thank you so very much for all you have done for our son, Kijana! He absolutely loved the recent trip to Tanzania. We thank you for giving him the opportunity to experience the rich culture of your home country. Kijana came back a different person--a better person--for all he was able to experience. You have given him a very valuable gift. He also truly enjoyed learning about Hemingway. thank you again for taking Kijana and the other students on the adventure of a life time. We hope to meet you sometime!
Sincerely,
Father and Mother of Kijana.
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Sababu moja ya kuuweka ujumbe huu hapa ni kwamba ni kielelezo cha manufaa yanayoweza kutokana na huu utaratibu uliopo katika vyuo vingi vya Marekani wa kupeleka wanafunzi nchi za nje. Inafahamika kuwa, mbali na somo wanaloenda kusoma, au masomo wanayoenda kusoma, ni fursa kwa vijana kupanua upeo wao wa kuifahamu dunia na tamaduni zake. Ni maandalizi kwa vijana hao kwa maisha yao ya baadaye katika ulimwengu huu unaoendelea kufungamana kwa kasi katika mchakato wa utandawazi.
Insha Allah, nitatafuta fursa nyingine nielezee faida ya programu hizi kwa nchi zinazowapokea hao wanafunzi, kama vile Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
2 comments:
hongera Profesa kwa mafanikio hayo Kiasi Kwamba wazaziwa wanafunzi wanatambua mchango wa safari hizo kwa maisha ya watoto hao ambao wana mtazamo tofauti kuhusu Afrika.
Nakutakia kazi njema
Asante Mkuu. Ni Mungu ndiye analeta hayo yote. Hii ni imani yangu. Kwa vile namtanguliza Mungu na kuwajibika kwa uwezo wangu wote katika shughuli hizi, naona mafanikio tena na tena.
Lengo moja la kusema hayo ni kuwapa moyo wengine, hasa vijana wetu.
Post a Comment