Tuesday, March 12, 2013

Mabucha, Mto wa Mbu

Nilipiga picha hii hapa kushoto kwenye mtaa mmoja wa Mto wa Mbu. Nilivutiwa na mwonekano huu: safu ya mabucha na pia akina mama wakiwa wamejitokeza tu hapo mlangoni  na kuelekea walikokuwa wanaelekea.

Nilitafakari suala la haya mabucha, ila sikupata fursa ya kuongea na yeyote kuhusu suala hilo. Sikuweza kujua kama wenye mabucha hayo ni akina nani.

Miezi mingi iliyopita, kulikuwa na taarifa za mgogoro Mto wa Mbu baina ya wa-Kristo na wa-Islam. Sikufuatilia undani wa tatizo, isipokuwa haikuwa taarifa njema, kwani migogoro si jambo jema.

Taarifa hii ilinigusa kwa namna ya pekee kwa sababu nilishafika Mto wa Mbu mara kadhaa na nafahamiana na baadhi ya watu wa pale. Mimi kama mgeni nilikuwa na hisia kuwa Mto wa Mbu ni mji uliotulia sana. Sikutegemea mgogoro wa aina ile. Hayo yote yalinijia kichwani wakati napiga picha hii.

1 comment:

Christian Sikapundwa said...

Nimefurahishwa na kazi yako ya kufuatilia matukio,Umzaie ndiye kumbe siye,ni sawa na matatizo yaliyojitokeza mto wa mbu,na hali ya utulivu uliyoikuta ni tofauti.
Jinsi unavyo weka kumbukumbu katika uhalisia,inapendeza,nimependezewa sana,Kanisa lile ni kama la Matogoro.kazi njema.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...