Monday, March 25, 2013

Toleo Jipya la "Kioo cha Lugha"

Siku chache ziilizopita, nilipata nakala ya jarida la Kioo cha Lugha, kutoka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mimi ni mwanakamati katika kamati ya uhariri wa jarida hilo. Ni furaha kubwa kwangu kushirikiana na wanataaluma wenzangu katika mambo ninayoyapenda. Masuala ya la lugha, fasihi, utamaduni, na falsafa yana nafasi ya pekee katika maisha yangu.Toleo hili la Kioo cha Lugha lina makala nyingi, kama inavyoonesha katika picha hii hapa kushoto. Wanaodhani kuwa ki-Swahili kina mapungufu katika kuelezea taaluma mbali mbali, watafakari upya suala hilo, hasa kwa kusoma machapisho kama yale yatokayo katika Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, ambayo ni ya taaluma mbali mbali. Niliwahi kugusia suala hilo katika ujumbe huu hapa.

No comments: