Juzi nilienda Lutheran Junior Seminary, Morogoro, kuangalia kitengo cha ufundishaji wa ki-Swahili na Utamaduni.
Kwa miaka mingi nilifahamu habari za kitengo hiki, kupitia mtandao wao, ila sikuwahi kuwatembelea. Nilifurahi kuonana na walimu na kutembezwa katika mazingira ya shule.
Kwa vile ninashughulika na program za kuleta wanafunzi wa Marekani hapa Tanzania na kwingineko Afrika, niliona ni muhimu nipate ufahamu mzuri wa kitengo hiki cha Morogoro, endapo tutahitaji kuwaleta wanafunzi wetu.
Nilitambulishwa kwa mwalimu ambaye alikuwa darasani akiwafundisha wageni somo la utamaduni. Kumbe anakifahamu kitabu changu cha Africans and Americans na anakitumia. Nilifurahi kuona kuwa niliyoandika yanawanufaisha wengi, hadi huku Morogoro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
8 comments:
Hapa ndipo nilipokulia. Nilifika hapo nikiwa na miezi kadhaa na nikakua hapo mpaka nilipofika darasa la 2. Ni kama nyumbani hapo
Napapenda na napakumbuka saana
Asante kwa taswira hizi
Ni kweli, pazuri sana hapa. Napangia kuwafikisha hapo wanafunzi ninaotegemea kwenda nao Tanzania mwakani, katika programu ya Lutheran Colleges Consortium for Tanzania.
Hakika sitasahau jinsi nilivyopata Elimu na Malezi na hata ule uwanja wa mpira wa miguu wa hapo LJS maana ni sehemu ya maisha yangu.
Kuna Waalimu wengi wazuri nawakumbuka na kuwashukuru sana kwa uwezo wao mzuri wa Kufundisha. Kipekee, leo nimtaje tu mmoja wao;
Mwl. Shilla (RIP) alivyokuwa wa kipekee. Mtu wa watu, Mweledi na aliyeweza kukonga nyoyo za Wanafunzi wake hususan katika maabara ya Fisikia mf. wakati anakokotoa ufanisi wa gurudumu kapi (efficiency of a pulley)kwa kutumia kikokoteo (a slide rule)!
kituo ni kizuri... nimesoma hapo kidato cha tano na sita.... kwa kweli nilipata malezi bora..ongera kwa mwalimu simtara
Ndugu Mkenda, nategemea kwenda tena hapo siku moja, ili nikafahamu vizuri zaidi habari zake, nipate kuendelea kuzitangaza. Katika dunia ya leo tuna fursa na uwezo wa kujitangaza duniani kote kwa kutumia tekinolojia mbali mbali za mawasiliano.
Ndugu Musuto wa Chirangi, shukrani kwa kutupa hizi taarifa za ziada.
hapo nimefundisha sana kiswahili wazungu Na waafrika.nilikuwa Na uwezo kumfundusha MTU WK tatu akaongea kiswahili safi
Ndugu Anonymous uliyeandika April 6, 2014 at 4:21 AM, nafurahi kusikia ulifundisha ki-Swahili katika chuo hicho. Kwa kweli hata huku ughaibuni, tunapoongelea taasisi za Tanzania ambazo ni maarufu kwa kuwafundisha wageni ki-Swahili, hicho chuo hakikosi kutajwa kama moja ya taasisi tatu au nne maarufu kabisa. Nikipata wasaa wa kutembelea tena, nitapenda kufanya mahojiano na wahusika, na pia kupiga picha, ili kuchapisha katika blogu hii na blogu ya ki-Ingereza.
Post a Comment