Thursday, August 19, 2010

Mkutano na Mwenyekiti Mjengwa


Juzi, tarehe 17 Agosti, nilipata fursa ya kukutana tena na mwanablogu maarufu, Maggid Mjengwa. Tulikutana Sinza, tukaongea kwa muda, kuhusu masuala mbali mbali.

Nilikutana na Mwenyekiti Mjengwa mara ya kwanza mwaka jana, kama ilivyoelezwa hapa. Juzi tuliongelea gazeti la Kwanza Jamii, ambalo yeye alilianzisha mwaka jana, nami nikawa mchangiaji wa makala. Tulibadilishana mawazo na kumbukumbu kuhusu yaliyotokea miongoni mwa wasomaji kuhusu gazeti hili, tukatathmini yale tuliyokuwa tunayakumbuka.

Nilikuwa na nakala ya kitabu changu cha CHANGAMOTO, ambacho ni mkusanyiko wa makala nilizoandika Kwanza Jamii. Mwenyekiti alifurahi sana kukiona, akanunua nakala kadhaa kwa ajili ya marafiki zake.

Alinieleza jinsi taasisi fulani kule Njombe ilivyopendezwa na gazeti la Kwanza Jamii, kiasi cha kufanya mkakati wa kuendeleza juhudi za lile gazeti. Hayo ni mambo ya baadaye, ambayo ni changamoto.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni jambo la kufurahisha sana kuona kila kukicha wanablog wanazidi kuonana na kubadilishana mawazo. Mnajua huku kublog mwisho wake kunatufanya tuwe wanandugu kamili. Ipo siku nami nitakutana na wana/mwanablog. Upendo Daima

Fadhy Mtanga said...

ni furaha sana kuona wanablog mkikutana. Nadhani blog imekuwa sasa kama dini fulani ama taifa fulani sijui. Lakini bila shaka mlikuwa na wakti mzuri sana.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndia mtanga, ni kama familia ya mtandaoni, ni furaha kukutana live pia

juhudi za kurudishwa kwanza jamii zinahitajika na ni muhimu kwetu sote, na zitekelezeka haraka iwezekanavyo

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...