Nafanya mipango ya kwenda Iringa kufuatilia habari za mwandishi Hemingway. Pamoja na kuishi na kuzunguka Afrika Mashariki, miaka ya 1933-34 na 1953-54, alitumia muda mwingi Tanganyika. Kumbe, alitumia wiki kadhaa Iringa ule mwaka 1954.
Habari hii ni ya kusisimua, kwa mtafiti. Mwanae, Mzee Patrick Hemingway anayeishi Montana, amekuwa akinipa taarifa na dokezo muhimu.
Safari kama hii, na kukaa Tanzania wiki tatu nne, itagharimu dola zisizopungua 4000. Lakini chuo changu kimeomyesha kiko tayari kugharamia.
Utafiti wa aina hii ni muhimu sana. Mbali na umuhimu wake kitaaluma,faida mmoja ni kuwavutia watalii. Laiti kama wa-Tanzania wagekuwa watu wanaothamini na kusoma vitabu. Tungeshirikiana vizuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
2 comments:
pole na baridi kali prof
Shukrani. Ni mbaya sijawahi kuona.
Post a Comment