Monday, January 6, 2014

Huenda Nitaenda Iringa Mwaka Huu Kufuatilia Habari za Hemingway

Nafanya mipango ya kwenda Iringa kufuatilia habari za mwandishi Hemingway. Pamoja na kuishi na kuzunguka Afrika Mashariki, miaka ya 1933-34 na 1953-54, alitumia muda mwingi Tanganyika. Kumbe, alitumia wiki kadhaa Iringa ule mwaka 1954.

 Habari hii ni ya kusisimua, kwa mtafiti. Mwanae, Mzee Patrick Hemingway anayeishi Montana, amekuwa akinipa taarifa na dokezo muhimu. Safari kama hii, na kukaa Tanzania wiki tatu nne, itagharimu dola zisizopungua 4000. Lakini chuo changu kimeomyesha kiko tayari kugharamia.

 Utafiti wa aina hii ni muhimu sana. Mbali na umuhimu wake kitaaluma,faida mmoja ni kuwavutia watalii. Laiti kama wa-Tanzania wagekuwa watu wanaothamini na kusoma vitabu. Tungeshirikiana vizuri.

2 comments:

Anonymous said...

pole na baridi kali prof

Mbele said...

Shukrani. Ni mbaya sijawahi kuona.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...