Friday, January 11, 2019

Wanachuo wa Gustavus Adolphus Wameenda Tanzania

Tareha 7, nilikwenda kukutana na wanachuo wa Gustavus Adolphus College ambao walikuwa wanaondoka kwenda Tanzania katika programu ya masomo. Hii ni programu ambayo imekuwepo miaka mingi. Wanafunzi wengi zaidi wanasomea uuguzi, na wanakwenda Tanzania ili kuelewa suala la uuguzi linakuwaje katika utamaduni tofauti na wa Marekani.

Nimekuwa nikialikwa kila mara kuongea nao kuhusu masuala ya tofauti za tamaduni kutokana na kwamba wanasoma kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, na tunapokutana wananiuliza maswali yatokanayo na niliyoandika au mengine. Maswali yalikuwa ya aina mbali mbali, yakiwemo kuhusu mtazamo wa waTanzania juu ya waMarekani na pia kuhusu hali ya kisiasa Tanzania.

Hapa kushoto ninaonekana na viongozi wa msafara, Profesa Barbara Zust na Mchungaji Tod Mattsn. Profesa Zust ndiye mwaandaji wa kozi na kila mwaka anaweka kitabu changu kama muhimu kwa wanafunzi. Silabasi yake mojawapo ni hii hapa https://gustavus.studioabroad.com/_customtags/ct_FileRetrieve.cfm?File_ID=01027"

No comments: