Saturday, November 9, 2013

Nimenunua "Nomad," Kitabu cha Ayaan Hirsi Ali

Miaka kadhaa iliyopita, nilianza kusikia jina la Ayaan Hirsi Ali, mwandishi kutoka Somalia, ambaye alikuwa ameikimbia nchi yake na alikuwa anaishi Uholandi, ambako alifanikiwa hata kuwa mbunge. Ilionekana ni mwandishi mkorofi, kwa maana ya kwamba wengi walikerwa na kukasirishwa alivyokuwa anahoji utamaduni wa wa-Somali na u-Islam, hasa kuhusu masuala ya haki za wanawake.

Nilisoma kuhusu kitabu chake Infidel, ambacho kilisemekana kiliwakasirisha wa-Islam wengi. Nilikuwa na dukuduku ya kusoma maandishi yake, lakini, kutokana na majukumu mengi, sikufuatilia.

Hata hivi, nimezingatia ukweli kuwa, kuliko kutegemea ya kuambiwa, muhimu mtu kujisomea mwenyewe. Leo nimenunua kitabu cha Ayaan Hirsi Ali kiitwacho Nomad. Ingawa ninasoma vitu vingi kila siku, nitakipa kitabu hiki kipaumbele. Wakati huo huo, nitanunua vitabu vyake vingine. Insh'Allah, nitapata wasaa wa kuelezea nawazo yake.

1 comment:

Mbele said...

Leo, tarehe 27 Machi, 2015, nimesoma Makala inayotoa mtazamo wa kufikirisha juu ya Ayaan Hirsi Ali. Mtu yeyote anayetafuta ukweli anategemewa kusikiliza kila hoja kwa makini. Makala yenyewe ni hii hapa.


Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...