Wednesday, May 11, 2022
Mpiga Debe Mpya
Siku mojawapo, baada ya mhadhara wangu juu ya "Money in African and American Culture," mhudhuriaji aitwaye Kelly aliweka picha ya vitabu vyangu kwenye ukurasa wake wa Facebook, pamoja na ujumbe huu:
Beautiful afternoon to sit in Miss Samantha's yard! I'm reading work from Joseph Mbele, suggested by my friend Anita. Joseph is leading a recurring Zoom call on Saturday mornings (10 to 11:30) with intriguing conversations, focusing on different topics. My inbox is always open, I'd be happy to share the next Eventbrite link.
Imetokea hivyo, kwamba tangu nianze programu hii, wahudhuriaji wamekuwa wapiga debe wangu wakuu. Wanawaambia wengine na kuwashawishi wahudhurie. Matangazo ya mada ninaweka Facebook siku chache kabla ya mhadhara. Yeyote anakaribishwa kujisajili kwa kutumia linki inayoambatishwa kwenye tangazo.
Monday, April 25, 2022
Mdau Wangu Makini Katutembelea
Mama huyu ni mdau wangu hodari, kwa maana kwamba ni msomaji wa tangu zamani wa vitabu vyangu na maandishi mengine, na ni mfuatiliaji wa shughuli zangu za kuelimisha jamii.
Kwenye haya matamasha, huwa sikosi kuwaona waAfrika wa nchi kama vile Somalia, Kenya, Ethiopia, Uganda, Sudani, Congo, Nigeria, Togo, Liberia au Ghana. Ninafurahi kuwa wadau kutoka nchi zote hizo wamenunua na wamevutiwa na kitabu changu kiitwacho Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.
Friday, March 18, 2022
Nimekutana na Mdau Wangu Mwingine
Nilikuwa nimemwomba tukutane, kwa sababu nilikuwa na mambo ya kumwuliza. Moja ni kuhusu uwezekano wa kujenga uhusiano baina ya shule za Osseo District na shule ya Bukoba, Tanzania, ambayo uongozi wake uliniomba niwatafutie uwezekano huo hapa Marekani..
Jambo jingine nililotaka kuongea naye ni muendelezo wa yale machache tuliyogusia siku ya mhadhara wangu, ambao yanahusu kuzuia au kutatua migogoro inyotokea shuleni. Tulikuwa tumakubaliana kwamba tofauti za tamaduni zinachangia tatizo hilo.
Jambo la tatu ni kuwa nilitaka kumpa nakala ya Chickens in the Bus: Embracing Cultural differences. Nilishampa Africans and Americans: Embracing Cultural Differences baada kukutana mara ya kwanza. Ilikuwa ni furaha leo kusaini hiki kitabu na kumkabidhi. Huyu namhesabu kama mdau wangu muhimu.
Tumeongea mengi yanayohusu shule, kuhusu migogoro mashuleni itokanayo na tofauti au changamoto za tofauti za tamaduni na kadhalika. Tumegundua kuwa kwa ujumla tuna mitazamo inayofanana. Tumekubaliana kushirikiana kwa dhati siku zijazo katika kutafuta njia za kutatua changamoto zilizopo.
Saturday, March 12, 2022
WADAU WA UTALII KWENYE MHADHARA WANGU ARUSHA
Friday, March 11, 2022
Vitabu Vinapatikana Kenya
Saturday, February 12, 2022
MTanzania Ughaibuni Aongelea Kitabu cha "Matengo Folktales"
Wiki hii, katika ukurasa wake wa Instagram, Coriona ameandika uchambuzi wake wa kitabu changu Matengo Folktales. Ameandika hivi:
I will start with a big smile. This book Matengo Folktales by John Mbele @africonexion. Took me way back into those days of story telling. Three stories in this book were so vividly. The Monster in the Rice, The Tale of two women and the Tale of Katigija. The sound of the songs in these stories is what I am still trying to remember. These songs were always sang with everyone when the stories were narrated. This is what is missing in story telling these days. We let our children just listen to the story without them taking part.
However, I am quite shocked with the amount of killing in every story. At least I don't remember the killing part. For example the Tale of two women, I remember this part when the woman was told to lick the wounds. And in Katigija Tale I remember the grandma singing when she brought the food to the child and the Monster in the Rice field, I remember how the children kept on disappearing.
My son was shocked when I told him The tale of Monster in the Rice. He was like, what a story, what a family 🙈🤣
Beautiful written and I like the comment section. This helps one to understand why these stories were what they were.
Now I need someone to sing those songs for me 🥳🤗
Nitaanza na tabasamu kubwa. Kitabu ni "Matengo Folktales" cha [Joseph] Mbele. Kilinirudisha kwenye siku zile za usimuliaji hadithi. Hadithi tatu katika kitabu hiki zilisisimua: “Jitu Katika Shamba la Mpunga,” “Kisa cha Wanawake Wawili” na "Hadithi ya Katigija.” Najaribu kukumbuka sauti za nyimbo katika hadithi zile. Nyimbo hizi daima ziliimbwa na wote wakati hadithi zinasimuliwa. Hicho ndicho kinachokosekana katika usimulizi wa hadithi leo. Tunawafanya watoto wetu wasikilize tu bila wao kushiriki.
Lakini, nimeshtushwa na idadi ya mauaji katika kila hadithi. Sikumbuki sawasawa sehemu ambapo mauaji yenyewe yanatokea. Kwa mfano, "Kisa cha Wanawake Wawili," nakumbuka pale mwanamke anapoambiwa kulamba vidonds. Na katika “Hadithi ya Katigija” nakumbuka bibi anavyoimba wakati anamletea mtoto Katigija chakula, na katika “Jitu Katika Shamba la Mpunga” nakumbuka jinsi watoto walivyokuwa wanapotea. Mtoto wangu alishtuka nilipomsimulia “Kisa cha Jitu Katika Shamba la Mpunga.” Alishangaa ni hadithi gani hiyo, na ni familia gani hiyo.
Wednesday, February 9, 2022
Vitabu Viko Chuoni Mbeya
Katika mhadhara wangu, niliibua masuala ambayo nimeyaongelea katika vitabu vyangu Africans and Americans: Embracing Cultural Differences na Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences. Lengo langu kuu lilikuwa kuanzisha jadi ya kutafakari changamoto za tofauti za tamaduni katika ulimwengu wa utandawazi wa leo.
Tafakari hii inapaswa iwe endelevu. Kuchangia hilo, nilikabidhi nakala za hivi vitabu vyangu viwili kwa ajili ya maktaba ya chuo. Baadaye mkurugenzi wa maktaba ameniandikia ujumbe wa shukrani kwa kupewa vitabu hivyo.
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Ukizunguka mitaani Dar es Salaam, utakuta matangazo mengi ya waganga wa kienyeji. Waganga hao wanatoka sehemu mbali mbali, kama vile Sumbaw...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Jina la Shaaban Robert ni maarufu miongoni mwa wa-Tanzania na wengine wa nchi zingine wanaokijua ki-Swahili. Lakini, tujiulize ni wa-Tanza...

