Saturday, May 23, 2020
Tuesday, May 19, 2020
Utalii wa Utamaduni Wilayani Kwetu
Kwa miaka na miaka nimekuwa nikiongelea masuala ya utamaduni na utandawazi pia utamaduni na utalii au utili wa utamaduni. Nimewahi kuhusisha vitabu na utalii. Nimesema kuwa watalii wengi kutoka huku ughaibuni, kama vile Marekani, hupenda kusoma vitabu, na sisi tutahitaji kuwa na maduka ya vitabu.
Napenda kujielekeza wilayani kwetu: wilaya ya Mbinga, lakini Nyasa pia. Tunatakiwa kuandika vitabu kuhusu historia, utamaduni, na mambo mengine ya kwetu. Watalii wakija, wakute maduka ya vitabu, vitabu kuhusu historia ya miji kama Mbambabay, Liuli, Lituhi, Mbinga, Kigonsera na kadhalika pia taasisi kama hospitali ya Litembo. Wakute vitabu kuhusu vivutio kama jiwe la Mbuji.

Tuwe na hifadhi ya vitu mbali mbali vya kitamaduni, kama vile mitumbwi, nyavu za kuvulia samaki, ala za muziki, kama vile ngoma, "ngwaja," "sekatela," "mapenenga," na "nkwendakwenda." Katika jumba la hifadhi, ziwepo video za ngoma, na masimulizi ya hadithi. Ziwepo picha za vivutio na watu mbali mbali wakiwa katika shughuli kama kulima, uvuvi, kusuka vikapu, kufinyanga vyungu, na kadhalika.
Watalii watafurahi kuangalia ngoma na vivutio, lakini wakipata vitabu, watajielimisha kuhusu waliyoyaona. Vitabu vinawezesha elimu endelevu. Kwa njia ya vitabu hivi, tutauelimisha ulimwengu. Vijana wetu nao wataelimika kwa kusoma vitabu hivi.

Sunday, May 3, 2020
Friday, May 1, 2020
Mhadhara Wangu wa Kwanza Kwa Zoom
Tarehe 28 mwezi huu, nilitoa mhadhara kwa wanachuo wa chuoni St. Olaf na wasikilizaji walikuwa Mankato. Mada ilikuwa Understanding Each Other: Brothers and Sisters From Two Continents.
Nimeshahutubia wanachuo wa South Central College mara kadhaa, na ninafurahi kuwa wanaendelea kuwa na hamu ya kunisikiliza, kama inavyoelezwa hapa. Kivutio kimojawapo ni kitabu changu
Hii tarehe 28 ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuhutubia kwa kutumia Zoom. Changamoto ya kuhutubia bila kuiona hadhira kiuhalisia haikosi kuathiri mhadhara. Lakini ripoti nilizopata kutoka kwa mratibu wa mhadhara ni kwamba watt waliufurahia mhadhara wangu, ambao ni huu hapa.

Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...