
Jennifer alisoma kitabu akaandika maoni kwa nyakati mbali mbali:
Ni kitabu murua chenyee upeo utakaowasidia waAfrika na waMarekani.
Uzoefu wangu unaendana na karibu kila kipengele kitabuni humu. Na kitawafungua macho watu wa tamaduni zote mbili.
Ninakipendekeza kitabu hiki kwa kila mmoja, akisome kwa sababu kitamgusa.
Jennifer nami tulikutana mtandaoni wiki chache zilizopita tukiwa wafuasi wa Toyin Umesiri, mhamasishaji maarufu wa biashara baina ya Afrika na Marekani, ambaye aliwahi kufanya mahojiano nami kuhusu kitabu changu na kuhusu athari za tamaduni katika biashara baina ya waAfrika na waMarekani. Jennifer ni mjasiriamali, mwanzishi na mkurugenzi mkuu wa Chiblenders Green. Katika juhudi za kueneza shughuli zake kimataifa, anafahamu umuhimu wa kuzielewa tamaduni za wengine. Katika muda mfupi wa kufahamiana naye, amenifundisha mengi na ninamshukuru.