Leo nilienda Mall of America kukutana na Tanya, mjumbe wa bodi ya shule za Osseo District. Tulifahamiana miezi kadhaa iliyopita, siku nipotoa mhadhara kwa Rotary Club of Brooklyn Park. Alikuwa mmoja wa wahudhuriaji, na nilimfahamu siku hiyo kama mjumbe wa bodi ya shule za Osseo District.
Nilikuwa nimemwomba tukutane, kwa sababu nilikuwa na mambo ya kumwuliza. Moja ni kuhusu uwezekano wa kujenga uhusiano baina ya shule za Osseo District na shule ya Bukoba, Tanzania, ambayo uongozi wake uliniomba niwatafutie uwezekano huo hapa Marekani..
Jambo jingine nililotaka kuongea naye ni muendelezo wa yale machache tuliyogusia siku ya mhadhara wangu, ambao yanahusu kuzuia au kutatua migogoro inyotokea shuleni. Tulikuwa tumakubaliana kwamba tofauti za tamaduni zinachangia tatizo hilo.
Jambo la tatu ni kuwa nilitaka kumpa nakala ya Chickens in the Bus: Embracing Cultural differences. Nilishampa Africans and Americans: Embracing Cultural Differences baada kukutana mara ya kwanza. Ilikuwa ni furaha leo kusaini hiki kitabu na kumkabidhi. Huyu namhesabu kama mdau wangu muhimu.
Tumeongea mengi yanayohusu shule, kuhusu migogoro mashuleni itokanayo na tofauti au changamoto za tofauti za tamaduni na kadhalika. Tumegundua kuwa kwa ujumla tuna mitazamo inayofanana. Tumekubaliana kushirikiana kwa dhati siku zijazo katika kutafuta njia za kutatua changamoto zilizopo.
Friday, March 18, 2022
Saturday, March 12, 2022
WADAU WA UTALII KWENYE MHADHARA WANGU ARUSHA
Tarehe 8 Januari, 2022, nilitoa mhadhara Arusha, mada ikiwa "challenges of cultural differences," yaani changamoto za tofauti za tamaduni. Hii ni mada ambayo naiongelea na kuiandikia sana.
Mwandaaji wa mhadhara alikuwa mama Ama, mMarekani Mweusi. Walihudhuria watu wa mataifa mbali mbali, lakini zaidi kutoka Marekani na Tanzania. Tuilkaa kwa takriban saa tatu.
Baadhi ya waTanzania waliohudhuria ni vijana wa kampuni ya utalii iitwayo Rift Valley Cultural Tourism, ambayo makao yake ni Karatu. Kupitia kwa mkurugenzi wa kampuni, wote walikuwa wamepata nakala za kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences," na walikuwa wamekisoma.
Waliposikia kuwa ninatoa mhadhara, waliamua kuhudhuria. Tulifurahi kukutana. Baada ya mhadhara, tulipiga hii picha inayoonekana hapa juu; baadhi yao wameshika kitabu changu.
Wadau wa utalii ni wanufaika wa moja kwa moja wa kitabu hiki. Hii ilidhihirika mwaka 2007 wakati mkurugenzi wa J.M. Tours aliponunua nakala kadhaa akawapa madreva waongoza watalii wake wasome.
Walikifurahia kwa msingi kwamba kiliwawezesha katika kushughulika na watalii. Niliandika kuhusu hilo kwenye makala yangu, "My Arusha Readers."
Ninawapongeza Rift Valley Cultural Tourism kwa kutambua fursa na kuitumia. Niko tayari kuwa nao bega kwa bega katika masuala ya utalii na utamaduni, kubadilishana uzoefu na kuelimishana.
Mbali ya vitabu vyangu, ambavyo vinapatikana mtandaoni, nawakaribisha kwenye chaneli yangu ya YouTube.
Friday, March 11, 2022
Vitabu Vinapatikana Kenya
Vitabu vyangu viwili, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences na Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences, vinapatikana Nairobi. Yeyote aliyeko Kenya anayevihitaji apige simu namba 0742 765 588.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...