Tarehe 30 Septemba, 2023, nilikwenda Maple Grove, Minnesota, kuongelea kitabu changu cha Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences. Kikao kilifanyika katika maktaba ya Maple Grove. Tulitambulishana na wale ambao hatukufahamiana. Tulibadilishana uzoefu na mawazo.
Aliyeandaa na kuendesha kikako ni Samba Fall wa Senegal aonekanaye kulia kabisa kwenye hii picha. Yeye ni mratibu wa Multicultural Kids Network pia mjumbe katika Hennepin County Race Equity Advisory Council. Yeye na mimi tumefahaiana kwa miaka kadhaa.
No comments:
Post a Comment