
Leo, tarehe 21 Desemba, 2023, nimepata habari ya pekee kuhusu kitabu cha
Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences. Mama mmoja kutoka Cameroon aishiye hapa Minnesota, na ni mmoja wa wale ambao wamafahamu kazi zangu miezi ya karibuni, ameniambia kuwa anahitaji nakala za
Chickens in the Bus kwa ajili ya kuzipeleka kwenye shule Cameroon, ambayo yeye mi mmoja wa wahusika. Amesema wanahitaji nakala 20 ili kila darasa liwe na angalau nakala tatu.
Taarifa hii imenifanya nirudie kukipitia kwa uangalifu kitabu hiki, nijiridhishe hakina kosa lolote. Naogopa kuwapa watoto wa shule kitabu chenye kosa. Kwa mtazamo wangu, kusambaza kitabu chenye makosa ni uhalifu. Kuwapa watoto kitabu cha namna hiyo ni kosa la jinai.