Sunday, July 18, 2021
Utamaduni wa waCheki
Jana, tarehe 17, nilienda Montgomery, nikapata fursa ya kuangalia hifadhi. Ina mambo mengi sana ya historia na utamaduni. Nilipiga nyingi. Hapa naleta baadhi.

Tuesday, July 13, 2021
Tamasha la Kimataifa Faribault, Minnesota
Tarehe 10 Julai, 2021, nilishitiki International Festival Faribault, tamasha linaloandaliwa na Faribault Diversity Coalition mara moja kwa mwaka. Safari hii, nilimwalika Bukola Oriola, mwenye asili ya Nigeria, na mwanae Samuel Jacobs kuwa nami kwenye meza yangu na vitabu vyao.
Niliwahi kuwa mwanabodi wa Faribault Diversity Coalition na nimeshiriki tamasha mara nyingi. Wanakuwepo watu kutoka mataifa mbali mbali. Bendera za nchi zao zinapepea hapa uwanjani siku nzima. Katika ratiba ya tamasha, kunakuwepo muda wa watu kuandamana wakiwa na bendera zao kuelekea jukwaa kuu, na hapo kila mmoja hupata fursa ya kuelezea kifupi bendera na nchi husika.

Monday, July 5, 2021
Jirani Yangu, Msomaji Wangu
Pichani katikati ni mama Merrilyn McElderry, na kushoto ni mjukuu wake. Nilijipiga picha hii nao juzi, tarehe 3 Juni, mjini Edina, jimbo la Minnesota.
Merrilyn ni mwalimu mstaafu, msomaji makini wa maandishi yangu. Anayapenda na anafuatilia kwa karibu shughuli zangu kuhusiana na hadithi na mihadhara.
Aliposoma kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, aliandika dondoo za kusisimua akifananisha utamaduni wa waAfrika na ule wa Wahindi Wekundu. Aliweza kufanya hivyo kirahisi kwa kuwa alishafanya kazi miaka 15 katika eneo wanamoishi waChippewa. Baraka iliyoje kwangu kuwa na wadau wa aina yake.
Sunday, June 27, 2021
Kitendea Kazi

Ukiona jembe limechakaa, ujue linatumika. Kitabu hiki ni sawa na jembe. Mashuhuda ni waMarekani wenye shughuli yoyote na waAfrika, pia waAfrika kama Abraham Thomas wenye shughhuli yoyote na waMarekani. Kinaepusha migogoro na kuchangia ufanisi.
Wednesday, June 23, 2021
KITABU KINAPATIKANA ARUSHA
Mjasiriamali wa Arusha anauza kitabu hiki ambacho kimekuwa gumzo huku nje ya Tanzania hadi hivi karibuni katika Trade With Africa Business Summit, mkutano uliohudhuriwa na watu maarufu kutoka nchi mbali kuanzia Umoja wa Afrika, hadi Israel, Ujerumani, Nigeria, Ghana, Afrika Kusini, na Marekani. Piga simu namba 0787 597 202
Sunday, June 13, 2021
Hitimisho la Trade with Africa Business Summit 2021
Video hii ni ya hitimisho la mkutano uliofanyika tangu Mei 31 hadi Juni 4, uitwao "Trade With Africa Business Summit." Nimeshautajataja mkutano huu hapa. Kila mtu alishukuru kwa kuhudhiria kutokana na elimu kubwa na pana iliyopatikana katika mihadhara na mijadala.
Mwaandaaji wa mkutano, Toyin Umesiri, alikuwa amenialika nikaongelee kitabu changu, "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences." Kitabu kilitajwatajwa kwenye mkutano, hata katika video hii ya dakika za mwisho za mkutano. Mtoa mada Vera Moore, mmiliki wa kampuni ya Vera More Cosmetics, anaonekana mwishoni kabisa akiwa ameshika kitabu. Tulishangaa amekipataje upesi namna ile.
Namshukuru Toyin kwa mwaliko wake. Ameniarifu kuwa ataendelea kunibebesha majukumu, nami niko tayari. Video zote za mkutano zinapatikana mtandaoni. Nikizingatia thamani ya elimu iliyomo, kulipia gharama iliyotajwa ni sawa na uwekezaji makini. Zinapatikana hapa: https://www.nazaru.trade/courses/5248326/content

Thursday, June 10, 2021
Nina Wasomaji Butiama kwa Mwalimu Nyerere
Sijawahi kufika Mwitongo, Butiama, lakini kitabu changu, ambacho ni kama nafsi yangu, kimefika. Pichani anaonekana mjukuu wa Mwalimu Nyerere akiwa anasoma kitabu hiki. Picha hii aliiweka mitandaoni akiwa ameambatisha ujumbe. Ninanukuu baadhi ya aliyosema."My Dad gave me this book to read this morning, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences by Joseph Mbele. I just finished it. One lesson I learned is to respect, understand, and see the value in both cultures. I would highly recommend this book." .................. "My Dad gave me this book, he felt that it could be helpful for me, I’ve lived in the US since I was 7, I’ve made the decision to move back this year. There are many things which I still question. It will be a long learning process, this book has given me hope." .................. "Thank you for writing this book Professor Mbele. I’ve learned quite a lot from reading it but I’ve also grasped a better understanding of many things which haven’t been clear to me before."
Naleta tafsiri yangu kwa kiSwahili:
"Baba alinipa kitabu hiki asubuhi hii nisome, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, cha Joseph Mbele. Nimemaliza sasa hivi. Jambo moja ambalo nimejifunza ni kuheshimu, kuelewa, na kuona thamani ya tamaduni zote mbili. Ninanipendekeza sana kitabu hiki."....
" Baba alinipa kitabu hiki, kwa kuona kwamba kingeweza kunisaidia. Nimeishi Marekani tangu nikiwa na miaka saba, na nimeamua kurejea nyumani mwaka huu. Kuna mambo mengi ambayo bado nayahoji. Itanichukua muda mrefu kujifunza; kitabu hiki kimenipa matumaini."....
"Asante kwa kuandika kitabu hiki Profesa Mbele. Nimmejifunza mengi kwa kukisoma na nimepata uelewa mzuri wa mambo mengi ambayo hayakuwa wazi kwangu."
Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Ukizunguka mitaani Dar es Salaam, utakuta matangazo mengi ya waganga wa kienyeji. Waganga hao wanatoka sehemu mbali mbali, kama vile Sumbaw...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Jina la Shaaban Robert ni maarufu miongoni mwa wa-Tanzania na wengine wa nchi zingine wanaokijua ki-Swahili. Lakini, tujiulize ni wa-Tanza...