Niko mjini Songea. Niliwasili jana jioni kwa basi kutoka Dar es Salaam. Mchana huu nimekuwa nikikata mitaa ya jiji letu hili la mkoa wa Ruvuma.
Nimepiga picha sehemu mbali mbali. Na leo hapa ninaziweka chache. Zingine nitaziweka baadaye, wadau wapate kujionea wenyewe taswira za jiji letu hili.
Wadau ambao mlifika Songea zamani mkija hapa sasa mtaona mabadiliko mengi.
Baada ya kuishi siku kadhaa Dar es Salaam, tukiteseka na mgao wa umeme, nimeshangaa kuona umeme uko siku nzima hapa Songea, na wenyeji wanasema hawana mgao wa umeme hapa. Wanashangaa habari hizi za Dar es Salaam.
Friday, July 29, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
10 comments:
Safari njema Mkuu! Na umenitamanisha kweli SOngea ambako ndiko nilianzia shule ya Msingi na kumalizia shule ya vidudu katika shule ya Roman Katholiki hapo mjini ambako tulikula sana buluga!
ukikatiza mitaa hapana shaka sehemu zingine zinakustaajabisha kutokana na maendeleo
Naona wivu. Oooo Tanzania!!!
Karibu sana nyumbani Prof. Bila shska hutoacha kutuletea baraka zako na sie wa Dar
Wadau asanteni. Ndugu Mwaipopo, nipangia kuwepo Mbeya tarehe 17 hadi 20 Agosti. Ankal Michuzi uko katika orodha yangu ya watu wa kuwatafuta Dar. Insh'Allah tutaonana hivi karibuni.
Salam and pole kwa safari Prof wangu. Kama utakuwepo Dar mpaka tar 25 August nitakutafuta maana nitakuwa hapo Dar kwa likizo fupi
Prof Mbele pole na safari.naomba usikose kuonana na kuwasiliana na Dr Rev Mwankenja pale chuo cha ualimu Mbeya-Uyole.Naamini namba yake ya simu unayo kama nilivyokupatia.Anakusubili kwa hamu na pia atapenda kuwaandalia usafiri wa kwenda Matema na pia kuwafanyia boking ya kulala Mbeya mkitoka Dar.
Mwalilino
safi sana, labda na mwaka huu tutakutana kama mwaka jana, salimia ya hukoyote
Karibu sana Songea nimepata habari zako kwa Dada Yasinta alikuwa hapa jana na mmewe kutembelea ofisi zatu za TUJIFUNZA alisema ulikuwa umeelekea nyumbani Litembo,Tupo uwanja wa sabasaba Matarawe Magazeti vijijini.Karibu simu yangu ni 0756 282368 Voda.
Prf.namba yangu ya Tigo ni 0652828964.Voda nimepoteza. leo,Habari za Mbamba - Bay karibu tena Songea.
Post a Comment