Friday, July 29, 2011

Niko Songea

Niko mjini Songea. Niliwasili jana jioni kwa basi kutoka Dar es Salaam. Mchana huu nimekuwa nikikata mitaa ya jiji letu hili la mkoa wa Ruvuma.
Nimepiga picha sehemu mbali mbali. Na leo hapa ninaziweka chache. Zingine nitaziweka baadaye, wadau wapate kujionea wenyewe taswira za jiji letu hili.

Wadau ambao mlifika Songea zamani mkija hapa sasa mtaona mabadiliko mengi.Baada ya kuishi siku kadhaa Dar es Salaam, tukiteseka na mgao wa umeme, nimeshangaa kuona umeme uko siku nzima hapa Songea, na wenyeji wanasema hawana mgao wa umeme hapa. Wanashangaa habari hizi za Dar es Salaam.

10 comments:

SIMON KITURURU said...

Safari njema Mkuu! Na umenitamanisha kweli SOngea ambako ndiko nilianzia shule ya Msingi na kumalizia shule ya vidudu katika shule ya Roman Katholiki hapo mjini ambako tulikula sana buluga!

John Mwaipopo said...

ukikatiza mitaa hapana shaka sehemu zingine zinakustaajabisha kutokana na maendeleo

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Naona wivu. Oooo Tanzania!!!

Michuzi said...

Karibu sana nyumbani Prof. Bila shska hutoacha kutuletea baraka zako na sie wa Dar

Mbele said...

Wadau asanteni. Ndugu Mwaipopo, nipangia kuwepo Mbeya tarehe 17 hadi 20 Agosti. Ankal Michuzi uko katika orodha yangu ya watu wa kuwatafuta Dar. Insh'Allah tutaonana hivi karibuni.

Emmanuel said...

Salam and pole kwa safari Prof wangu. Kama utakuwepo Dar mpaka tar 25 August nitakutafuta maana nitakuwa hapo Dar kwa likizo fupi

Anonymous said...

Prof Mbele pole na safari.naomba usikose kuonana na kuwasiliana na Dr Rev Mwankenja pale chuo cha ualimu Mbeya-Uyole.Naamini namba yake ya simu unayo kama nilivyokupatia.Anakusubili kwa hamu na pia atapenda kuwaandalia usafiri wa kwenda Matema na pia kuwafanyia boking ya kulala Mbeya mkitoka Dar.

Mwalilino

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

safi sana, labda na mwaka huu tutakutana kama mwaka jana, salimia ya hukoyote

Christian Sikapundwa said...

Karibu sana Songea nimepata habari zako kwa Dada Yasinta alikuwa hapa jana na mmewe kutembelea ofisi zatu za TUJIFUNZA alisema ulikuwa umeelekea nyumbani Litembo,Tupo uwanja wa sabasaba Matarawe Magazeti vijijini.Karibu simu yangu ni 0756 282368 Voda.

Christian Sikapundwa said...

Prf.namba yangu ya Tigo ni 0652828964.Voda nimepoteza. leo,Habari za Mbamba - Bay karibu tena Songea.