Tuesday, December 10, 2013

Kwa Wapumbavu wa Kigoma Wanaoleta Vurugu Kwenye Mikutano ya Dr. Slaa

Huu ni ujumbe kwenu wapumbavu wa sehemu mbalimbali za Kigoma ambao mmekuwa mkileta vurugu kwenye mikutano ya Dr. Slaa, katibu mkuu wa CHADEMA.

Ni moja ya haki za binadamu kutafuta, kupata, au kusambaza taarifa na mitazamo katika masuala mbali mbali yanayoihusu jamii. Someni tangazo la kimataifa la haki za binadamu. Taarifa hizo hupatikana kwa namna mbalimbali, kuanzia vyombo vya habari hadi mikutano.

Nimeona picha za makundi ya watu wakiwa wamekusanyika kumsikiliza Dr. Slaa. Hiyo ni haki yao, mojawapo ya haki za binadamu. Lakini nimeona pia taarifa za wapumbavu wachache, kama vile Kasulu, wakija kuvuruga au kujaribu kuvuruga mikutano hiyo. Hao ni wapumbavu. Kenge wakubwa.

CCM, chama ambacho kimeshika hatamu katika nchi hii, chenye wajibu wa kuongoza na kuelimisha jamii, kimekaa kimya. CCM naijumlisha katika kundi hili la wapumbavu. Zito Kabwe, ambaye anatajwa na hao wavurugaji kwamba wanamtambua yeye, naye hajasema kitu. Naye ni mpumbavu.

Kuna haki zingine za binadamu zinazohusika katika suala hili. Moja ni haki ya kila binadamu kukusanyika na kujumika na wengine kwa amani. Nyingine ni haki ya kila raia kwenda popote katika nchi yake. Wapumbavu wa Kigoma mjini waliomtishia Dr. Slaa asikanyage Kigoma wakapimwe akili.

Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa. Ila nakerwa na upumbavu nilioelezea.

4 comments:

Anonymous said...

Naona umekuwa mkali sana siku hizi, hawa unaowaita wapumbuavu, ni wapumbavu kweli, hawajui walifanyalo. Lakini wengi nahisi wamelipwa, wala sio kiasi kikubwa, kwa hisia zangu hazidi hasa shs 10,000

Anonymous said...

Sioni kama ni wapumbavu zaidi ya watu wenye njaa. Hitimisho la kuwaita wapumbavu ni la haraka sana. Linaweza kutoa nafasi kwao kukuita wewe mpumbavu bila sababu. Punguza munkari prof. Nadhani usomi si kupayuka bali kuchungua mambo na kujenga hoja badala ya matusi. Ni ushauri tu.

Mbele said...

Blogu hii ya hapakwetu ni huru. Hatulindani hapa wala kuoneana haya. Nildhani nimetoa hoja, nikaelekeza watu kwenye vipengele vya haki za binadamu vilivyohujumiwa.

Hata hivi, mwenye hoja za kupinga hoja zangu anakaribishwa. Atakuwa ametuelimisha, au niseme atakuwa amenielimisha

mandela pallangyo said...

Kweli mtu asiyezingatia ustaarabu. Ni mpumbavu tuu. Hakuna namna ya kumuita. TUMUITE MTUKUFU?

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...