

Mmiliki na mkurugenzi wa African Travel Seminars, Georgina Lorencz, aliniagiza nipeleke nakala za kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, ambacho siku za karibuni ameanza kukipendekeza kwa wadau naowapeleka Afrika. Nilipeleka pia nakala za Matengo Folktales kuwa kuwa nilijua kuwa katika hotuba yangu ningetaja umuhimu wa kuelewa misingi ya utamaduni na falsafa ya wahenga wetu wa Afrika.

Kulikuwa pia na vyakula vha kiAfrika.


Washindi walipewa zawadi, zikiwemo nakala za kutabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Georgina alikuwa ameagiza kuwa kilt mtu agenda akita ameba vazi la kiAfrika. Nami nilijiandaa kwa kununua shati siku mbili kabla ya tukio, kwa sababu mashati yangu mengine nimeshayavaa mara kwa mara miaka iliyopita.

Palifanyika mashindano ya mavazi kwa lengo la kumtambua mtu aliyetia fora kwa vazi la kiume na hivyo hivyo kwa vazi la kike. Nilipata fursa ya kuongea na watu kadhaa, nikajionea wnavyipenda kampuni ya African Travel Seminars.

Niliona pia watu walivyovutiwa na yale niliyosema, kwa jinsi walivyochangamkia vitabu vyangu na kuvinunua. Mwishoni mwa sherehe, Georgina alitabgaza mipango ya safari zijazo mwaka huu mwezi Septemba na mwakani kwenda Afrika Kusini na Brazil.

No comments:
Post a Comment