Tarehe 12 Januari, 2024, nilisafirisha vitabu vyangu viwili, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences na Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences, kwenda Tehran, Iran, kwa mwendesha kipindi cha televisheni kiitwacho THE ENLIGHTENMENT SHOW. Hii ilikuwa ni baada ya yeye kufanya mahojiano nami, akiwa amelenga zaidi kwenye mada ya fasihi ya Afrika na ukoloni, na pia mitazamo ya waMarekani kuhusu Afrika.
Mahojiano tulifanya kwa Zoom, na hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kufanyiwa mahojiano Iran. Ninasubiri kwa hamu kupata mrejesho kutoka kwa watu wa kule, hasa baada ya vitabu vyangu kuwafikia.
Sunday, January 14, 2024
Sunday, January 7, 2024
NIMEKABIDHI “CHICKENS IN THE BUS”
Januari 4, 2024, nilikwenda Maple Grove, kukabidhi nakala 20 za Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences kwa mama wa Cameroon ambaye alikuwa ameziagiza kwa ajili ya shule fulani nchini Cameroon.
Katika maongezi, mama huyu alinieleza habari za shule yenyewe, ambayo iko kaskazini magharibi mwa Cameroon, uliko mji wa Bamenda. Alinieleza kwamba lengo lake ni kuwa hivi vitabu visomwe na wanafunzi wa darasa la sita kwenda juu.
Tuliongelea umuhimu wa kuwafundisha watoto wa kiAfrika juu ya utamaduni wetu, na kuwajenga katika kuuheshimu. Huyu mama alisisitiza kuwa yaliyomo katika Chickens in the Bus yanakidhi malengo hayo.

Mimi kama mwandishi nafurahi sana kujua kuwa watoto wa kiAfrika watakuwa wanasoma na kutafakari kitabu changu
Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...