 Januari 4, 2024, nilikwenda Maple Grove, kukabidhi nakala 20 za Chickens in the Bus: More Thoughts on Cultural Differences kwa mama wa Cameroon ambaye alikuwa ameziagiza kwa ajili ya shule fulani nchini Cameroon.

Katika maongezi, mama huyu alinieleza habari za shule yenyewe, ambayo iko kaskazini magharibi mwa Cameroon, uliko mji wa Bamenda. Alinieleza kwamba lengo lake ni kuwa hivi vitabu visomwe na wanafunzi wa darasa la sita kwenda juu.
Tuliongelea umuhimu wa kuwafundisha watoto wa kiAfrika juu ya utamaduni wetu, na kuwajenga katika kuuheshimu. Huyu mama alisisitiza kuwa yaliyomo katika Chickens in the Bus yanakidhi malengo hayo.
Mimi kama mwandishi nafurahi sana kujua kuwa watoto wa kiAfrika watakuwa wanasoma na kutafakari kitabu changu 
 
No comments:
Post a Comment