Nimewahi kuandika kuwa kama mwandishi, najikuta nikialikwa kuongelea maandishi yangu, na pengine kuongelea kitabu maalum. Hayo niliandika katika blogu hiiWakati mwingine, mwandishi unaalikwa kwenye mahojiano katika vyombo vya habari. Nami nimewahi kuhojiwa katika redio, blogu, na magazeti.
Hapa naleta mahojiano niliyofanyiwa mwaka 2006 na m-Tanzania Deus Gunza, ambaye alikuwa anamiliki na kuendesha Radio Butiama, kule Columbus, Ohio. Mahojiano hayo ya papo kwa papo yalihusu kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Yasikilize mahojiano haya hapa:
http://butiama.podomatic.com/entry/2006-09-02T06_26_37-07_00