Nimewahi kuandika kuwa kama mwandishi, najikuta nikialikwa kuongelea maandishi yangu, na pengine kuongelea kitabu maalum. Hayo niliandika katika blogu hii
Wakati mwingine, mwandishi unaalikwa kwenye mahojiano katika vyombo vya habari. Nami nimewahi kuhojiwa katika redio, blogu, na magazeti.
Hapa naleta mahojiano niliyofanyiwa mwaka 2006 na m-Tanzania Deus Gunza, ambaye alikuwa anamiliki na kuendesha Radio Butiama, kule Columbus, Ohio. Mahojiano hayo ya papo kwa papo yalihusu kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Yasikilize mahojiano haya hapa:
http://butiama.podomatic.com/entry/2006-09-02T06_26_37-07_00
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
4 comments:
Prof Mbele nimekusikiliza vizuri na nimekuelewa. Nina swali moja. Jee una mpango wa kutoa muendelezo wa kitabu chako?
Ndugu Malifa Michael, shukrani kwa ulizo lako. Katika taaluma, hakuna hitimisho. Kitabu cha aina hii huwa ni mwendelezo wa tafakari na pia kichocheo cha tafakari zaidi.
Unaandika kitabu ili tu kurekodi hatua uliyofikia katika safari yako, lakini safari yenyewe haiishi. Hakuna kulala, wala hakuna kujiaminisha kuwa kazi umemaliza.
Ninayatafakari masuala husika muda wote, na ninapoalikwa kutoa mihadhara Napata fursa ya kuendeleza tafakari, kuelezea au kufafanua vipengele ambavyo havikugusiwa au kufafanuliwa kitabuni.
Kwa miaka kadhaa, pamoja na hiyo mihadhara, na mazungumzo mbali mbali na watu, nimekuwa katika kuandaa kitabu kingine.
Na hicho kitabu kingine hakitakuwa hitimisho, bali mwendelezo tu.
Kila kitu ni muendelezo. Kwa ki-Ingereza wanaita "process." Kile tunachokidhania kuwa hitimisho, nacho ni sehemu ya hii "process."
Asante Prof Mbele kwa majibu yako mazuri na ya kufundisha pia. Nina swali moja. nikitumia kiswahili cha mtaani nina swali la kizushi. Prof najua umeandika vitabu vyingi. Ila hiki kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. unakizungumzia sana sana kuliko vitabu vyingine vyako. Unakipa airtime kubwa sana kwenye social network.. kwenye mihadhara etc
Je kwanini umeamua/unapenda kukizungumzia sana hiki kitabu kuliko vitabu vingine ambayo umeshawahi kuviandika?
Asante
Ndugu Malifa Michael, shukrani kwa ujumbe na ulizo lako. Kuuliza si ujinga.
Kati ya vitabu vyangu, ninakizungumzia zaidi hiki kimoja kutokana na ukweli kwamba asili mia kubwa ya mialiko ninayopata inahusiana na kitabu hiki, na kwenye hii blogu yangu na ile ya ki-Ingereza huwa naweka kumbukumbu ya matukio hayo.
Huenda siku moja nitaamua kuandika historia ya kitabu hiki, kuelezea mambo kama asili yake, jinsi nilivyoandika, na jinsi kilivyopokelewa katika jamii. Kumbukumbu hizi ninazoandika ni muhimu.
Ninaposema jamii, napenda nifafanue kuwa wasomaji wangu kwa ujumla ni wa-Marekani. Siwazuii wengine, ila kuna ule usemi kuwa ukiwa na siri, iweke kitabuni....
Post a Comment