Sunday, November 9, 2014

Nililazwa Tena Hospitalini

Kwa siku kadhaa, sikuandika chochote katika blogu zangu: hii na ile ya ki-Ingereza. Inapokuwa hali ni hiyo, wasomaji hujiuliza kuna nini.

Nilikuwa nimelazwa tena, kwa wiki moja, katika hospitali ya Allina Abbott Northwestern, kule Minneapolis.

Baada ya kuachiwa, nimekuwa nikipumzika. Kesho nategemea kuanza tena kufundisha. Chuo ambacho ni mwajiri wangu, kwa maelekezo ya daktari, kimenipunguzia sana majukumu, kuliko hata nilipoachiwa kutoka hospitalini miezi kadhaa iliyopita.

Nitakuwa nafundisha kozi moja tu, "South Asian Literature."

Mungu ni mkubwa na madaktari wanajua wanachofanya. Wananiambia kuwa hatimaye, hata kama ni baada ya miezi kadhaa, wana imani watayatatua matatizo ya afya yangu. Baada ya kurekebisha  matatizo mengine, sasa wanashughulikia figo. Wamenihimiza niendelee kufundisha, wakati wao wanashughulikia matatizo hayo.

Kama kawaida, nawashukuru wote wanaonikumbuka katika maombi na salaam. Nimeona nilete taarifa hii, kuelezea hali yangu, na kwa kuzingatia ukimya uliokuwepo kwa mwezi na siku kadhaa katika blogu zangu.

6 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kaka Mbele pole sana kwa kulazwa na hongera kwa kutoka hospitalini. Umefanya la maana kutujulisha nduguzo tofauti na watawala wetu wanaoficha hata kuugua utadhani hakuna binadamu asiyeugua.
Nilikuwa nikipita kibarazani bila kukuta kitu nikadhani kwa vile ulikuwa nje ya darasa kwa muda mrefu ulikuwa umejifungia darasani angalau kuwarejesha vijana ulipopaswa kuwafikisha kumbe ulilazwa tena! Mungu ni mkubwa atazidi kukupa nafuu na madaktari atawapa nuru waone jinsi ya kukuganga ipasavyo.
Nakutakia upone haraka na kuwa na siha njema kama siku zote. Aaaaaamini.

Anonymous said...

Pole sana Professor Mbele, Mungu akurejeshee afya na nguvu mapema

Mbele said...

Asante sana, ndugu yangu Mhango, kwa maneno yako ya busara na yenye kutia moyo. Sina la kuongeza bali kukutakia kila la heri.

Mbele said...

Shukrani tele, ndugu Anonymous.

Anonymous said...

Pole sana Joseph Mbele, nimekuwa napita hapa mara kwa mara nakuta kimya nikawa nahofu, pole sana

Mbele said...

Shukrani, anonymous uliyeandika tarehe 13 Novemba, kwa ujumbe wako. Naendelea kupona, na nafurahia kuwemo tena darasani, ingawa nafundisha kozi moja tu kwa sasa. Mungu akipenda, hatimaye nitapona kabisa. Nakutakia kila la heri.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...