Friday, October 6, 2017

Mkutano wa Africa Network Chuoni St. Olaf

Tarehe 29 September hadi 1 Oktoba, palifanyika mkutano wa Africa Network, hapa chuoni St. Olaf. ambapo ninafundisha. Africa Network ni jumuia ya vyuo vyenye kujihusisha na uendelezaji wa masomo kuhusu Afrika, katika taaluma mbali mbali. Jumuia hiyo ilianzishwa mwaka 2004 na watu wachache  kutoka vyuo mbali mbali, na mwaka hadi mwaka imekuwa ikivutia watu kutoka vyuo vingine.

Tumekuwa tukifanya mikutano ya mara kwa mara. Miaka ya mwanzo tulikuwa tukifanya mkutano kila mwaka, lakini miaka michache iliyopita tuliamua kuwa tukutane mara moja katika miaka miwili.

Katika mkutano wetu wa mwaka 2015, nilipendekeza kuwa mkutano wa mwaka huu ufanyike hapa chuoni St. Olaf. Kwa hivyo, nilibeba jukumu la kufuatilia kwa karibu kila kipengele cha maandalizi hayo, na hatimaye tumefanya mkutano kwa mafanikio makubwa.

Tumejadili mada mbali mbali zilizowasilishwa, tukabadilishana uzoefu na mikakati kuhusu ufundishaji. Tumejadili mipango na mikakati ya kupeleka wanafunzi Afrika kimasomo na changamoto  zake. Tumejadili sio tu masuala ya ufanisi bali pia maadili katika shughuli hizo.

Baadhi ya wahudhuriaji ni wa tangu zamani, lakini wengi walikuwa wapya. Tumefanikiwa kuwavuta watu kutoka vyuo vya mbali, hadi Afrika Kusini, ambao wako Marekani kwa wakati huu. Tumejifunza na tumefundishana mengi, na pia tumejengea mahusiano mapya yatakayotupeleka mbele katika shughuli zetu.


No comments:

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...