Leo nilikuwa mjini Faribault kushiriki tamasha la kimataifa International Faribault Festival. Nimeshiriki tamasha hilo kwa miaka kadhaa kama mwalimu, mwandishi, na mtoa ushauri kuhusu masuala ya tofauti za tamaduni.
Hapa kushoto ni wanafunzi waliokuwa wanaongoza shughuli katika ukumbi mkuu wa tamasha. Shughuli hizo zilikuwa ni maonesho ya burudani, hasa ngoma za mataifa mbali mbali.
Watu wa kila rika walihudhuria, kama ilivyo kawaida katika matamasha haya hapa Marekani. Kulikuwa ni michezo mbali mbali ya watoto.
Nilikwenda na vitabu vyangu na machapisho mengine, kama inavyoonekana picha ya mwisho hapa kushoto. Kama kawaida, vitu hivyo huwa ni kivutio kwa watu na wanafika hapa mezani kuangalia na pia kuongea nami. Hiyo leo ilikuwa ni hivyo hivyo. Niliongea na watu wengi, kuanzi watoto hadi wazee.
Kwa mfano, huyu bibi anayeonekana kulia, mwenye nywele nyeupe, tuliongea sana. Alinieleza kuwa anamfadhili binti yatima aliyeko Ethiopia. Tuligusia tofauti za tamaduni, nikamweleza jinsi ilivyo muhimu kuzitafakari, kwani zinaathiri tabia, mawasiliano, na mengine.
Mama mwingine aliyekuja hapa mezani pangu alisema anafundisha ki-Ingereza kwa wahamiaji kutoka nchi mbali mbali. Hapa Marekani, program hii inajulikana kama ESL, ambayo kirefu chake ni English as a Second Language. Basi, tuliongelea kidogo jinsi tofauti za tamaduni zinavyojitokeza katika programu hiyo, akanunua kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment