Aliniambia kuwa alifurahi sana kumsikia profesa akisema kuwa kitabu kimeandikwa na mTanzania. Alipiga picha kama kumbukumbu akawapelekea marafiki nyumbani. Kijana aliendelea kuniambia: "Nakupa hongera sana na mimi hii kwa njia moja ama nyingine imenitia nguvu ya kuendelea kusoma kwa bidii nifikie angalau nusu yako!"
Ninafurahi kuwa nimeweza kumtia kijana huyu hamasa ya kusoma kwa bidii. Kwangu kama mwalimu, haya ni mafanikio mazuri. Jambo mojawapo lililotamkwa katika "Azimio la Arusha" kuhusu mapinduzi yaliyokusudiwa Tanzania ni kwamba kazi iwe jambo la kujivunia. Nami najivunia kazi yangu.Vitabu vyangu kutumiwa katika vyuo vikuu si jambo geni kwangu. Vinatumiwa katika vyuo vya Marekani mara kwa mara. Lakini hii ni mara yangu ya kwanza kufahamu kuwa kitabu changu kinatumika China. Nimefurahi.
Ninamshukuru Seleman kwa kuniletea taarifa hii na kuniruhusu kuichapisha.

4 comments:
Heshima kwako professor
Shukrani kwa ujumbe wako. Pamoja na kufurahia taarifa hizi za ughaibuni, natamani jamii nchini mwangu izinduke na kuanza kutafakari masuala haya ya athari za tofauti za tamaduni katika ulimwengu wa utandawazi wa leo.
kitabu chako kinapatikana wapi
Ndugu Raman, kitabu hiki kinapatikana patika duka la Kimahama Literature Center (Arusha) na duka liitwalo A Novel Idea lililopo Slipway, Msasani. Vile vile kinapatikana mtandaoni.
Post a Comment