

Katika kunitambulisha kwa watu waliohudhuria, ndugu Schumacher aliwaelezea jinsi kitabu changu cha Matengo Folktales kilivyokuwa kimetajwa katika programu ya television ya Jeopardy Hiyo ni programu maarufu hapa Marekani.
Mhadhara wangu ulihusu chimbuko na kukua kwa utamaduni na tofauti za tamaduni. Niliongelea Afrika kama chimbuko la binadamu, lugha na masimulizi, kisha nikaelea jinsi kutawanyika kwa wanadamu sehemu mbali mbali za kulivyoleta tamaduni na lugha mbali mbali.

Wahudhuriaji walichangia mifano ya tofauti za tamaduni ambazo wamewahi kukumbana nazo. Mmoja alisema kwamba ni mwalimu na kwamba ana wanafunzi anaowapeleka Tanzania hivi karibuni. Nilifurahi kusikia hivyo.
Tulipomaliza kikao, watu walinunua vitabu vyangu nilivyoleta. Huyu mwalimu niliyemtaja alisema atavitumia vitabu hivi kama mwongozo kwa wanafunzi katika safari yao. Ninafurahi kwamba vitabu vyangu sasa viko katika maktaba ya AME Allen Church. Hili ni jambo kubwa, nikizingatia historia ya jengo hili ambalo lilijengwa mwaka 1885 na watu weusi baada ya kukombolewa utumwani.
No comments:
Post a Comment