Wednesday, August 12, 2020
Duka Jipya la Vitabu Vyangu
Mwanzilishi na mwendeshaji wa taasisi hiyo, Dr. Artika Tyner, ni profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha St. Thomas hapa Minnesota. Aliniuliza iwapo nitaridhia vitabu vyangu kuuzwa na taasisi hiyo.
Alianza kukifahamu kitabu changu mwaka juzi, baada ya kununua nakala kadhaa kwa ajili ya watu aliowapeleka Ghana katika safari ya kielimu akishirikiana na Monica Habia, mwanazuoni mwenzake kutoka Ghana. Baada ya safari hiyo, Monica alinielezea jinsi kitabu kilivyowasaidia waMarekani kuyaelewa mambo waliyokutana nayo Ghana.
Unaweza kutembelea tovuti ya Planting People Growing Justice. Vitabu hivi viwili vinapatikana Tanzania, katika maduka ya Soma Book Cafe na A Novel Idea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment