Sunday, December 13, 2020
Sunday, November 29, 2020
Hata Balozi wa Japani Kalalamikia Uchaguzi wa Tanzania
Ule unaoitwa uchaguzi ambao ulifanyika Tanzania tarehe 28 mwezi Oktoba umelalamikiwa sana ndani na nje ya nchi. Kilichonishtua zaidi ni kuwa hata Balozi wa Japani nchini Tanzania amelalamika, kwa tamko hili:
I am troubled by the information of widespread irregularities and wrongdoings during the recent election process in this country. I am convinced that sound democracy based upon multiparty system works best to contribute to further development and prosperity of Tanzania.
(GOTO Shinichi, Ambassador of Japan to Tanzania)
Ziko nchi, kama vile Marekani, ambazo tamaduni zao hazina utata juu ya kukosoa, kulalamika, na hata kukemea. Lakini Japan haina jadi hiyo, kwa misingi ya utamaduni wao ambao umejengeka katika dhana kama "saving face." Ukilalamikiwa na Japani, lazima ujitafakari sana, na hapa ndipo mamlaka za Tanzania zimekwama.
Niliwahi kutamka katika ukurasa wangu wa Facebook kuwa mimi kama mtafiti wa tofauti za tamaduni nililichukulia tamko la balozi wa Japani kwa uzito wa pekee kwa mujibu wa utamaduni wao, nikataja kitabu katika maktaba yangu cha utamaduni wa Japani, kilitwacho "Culture and Communication," ambacho kinaonekana pichani.
Baadaye, nilifukua maktaba yangu, nikaona vitabu vingine viwili, vinavyoonekana pia pichani. Katika kuvisoma, nimejithibitishia lile wazo langu kuwa kama hata Japani inalalamika, basi hujuma zilizofanyika katika uchaguzi lazima zilikuwa mbaya kupindukia. Nakaribisha mchango wa yeyote mwenye ujuzi na elimu zaidi, kwani hili ni suala la kitaaluma, na utafiti hauwekewi mipaka.
Thursday, November 26, 2020
Wednesday, November 25, 2020
Kitabu Kujadiliwa Chuoni St. Olaf
Tarehe 8 Januari, kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kitajadiliwa katika semina ya maprofesa wa chuo cha St. Olaf Nitaendesha hiyo semina ili kuleta mitazamo mipya juu ya migogoro ambayo waMarekani wana jadi ya kuijadili kama matokeo ya ubaguzi wa rangi. Suala la tofauti za tamaduni hawaliwazii. Semina yangu italenga kuleta dhana hiyo. Semina hii ni moja ya semina zinazoendeshwa kwa ufadhili wa Institute for Freedom and Community hapa chuoni. Kwa kawaida, semina hizi zinahusu mada za kitaaluma. Lakini hii semina yangu inahusu mahusiano ya watu ya kila siku, bila kupotelea kwenye mawingu ya nadharia. Profesa moja mstaafu, maarufu katika taaluma ya falsafa, baada ya kukisoma kitabu changu aliniambia kuwa tunahitaji kitabu cha aina hii.
Hii ni fursa ya kukitaambulisha kitabu changu rasmi hapa chuoni, ingawa kuna watu ambao wamekuwa wakikisoma.
Saturday, November 21, 2020
Alex Trebek wa "Jeopardy" Afariki
Alex Trebek, mwendeshaji wa kipindi cha televisheni cha "Jeopardy" amefariki, akiwa na miaka 80. Kwa hapa Marekani, "Jeopardy" ni kipindi maarufu sana, ila mimi sikuwa najua. Nilikuja kuzinduka tarehe 23 Novemba, 2017. Kumbe siku hiyo Trebek alikitaja kitabu changu Matengo Folktales katika kipindi chake. Watu mbali mbali walioshuhudia walianza kupeana na taarifa na mimi nikazipata. Pongezi zilifika kwa wingi, na ndipo nami nikafahaamu maana ya kutajwa kwenye kipindi hicho.
Saturday, October 31, 2020
Sunday, October 11, 2020
Tamasha la Kimataifa Faribault, Minnesota
Jana, tarehe 10, nilishiriki tamasha la kimatafifa mjini Faribault, Minnesota. Tamasha hilo huandaliwa kila mwaka na Faribault Diversity Coalition. Miaka iliyopita, nilikuwa mjumbe wa bodi wa hiyo Coalition.Tamasha hujumuisha maonesho ya tamaduni za watu wa mataifa mbali mbali waishio Faribault na maeneo ya jirani. Nimeshiriki tamasha hili Miaka iliyopita, na daima, inakuwa ni fursa nzuri ya kukutana na watu na kubadilishana uzoefu na mawazo kuhusu mambo mbali mbali ya dunia yetu ya utandawazi wa leo. Ninashiriki kama mwandishi na mtoa ushauri katika masuala ya taamaduni. Ninaonesha vitabu vyangu. Hii jana nilionesha pia vitabu via Bukola Oriola na mtoto wake wa miaka kumi na tatu Samuel Jacobs.


Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Ukizunguka mitaani Dar es Salaam, utakuta matangazo mengi ya waganga wa kienyeji. Waganga hao wanatoka sehemu mbali mbali, kama vile Sumbaw...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Jina la Shaaban Robert ni maarufu miongoni mwa wa-Tanzania na wengine wa nchi zingine wanaokijua ki-Swahili. Lakini, tujiulize ni wa-Tanza...

