Saturday, July 25, 2009

Taifa la Kesho

Wahenga walisema, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Picha hii inatueleza mengi kuhusu malezi ya watoto katika jamii yetu. Ni kawaida kwa watoto katika Tanzania kuonekana kwenye baa, na kwenye miziki, hata usiku wa manane. Humo mitaani wanashuhudia mambo ya ajabu mengi, kuanzia ulevi, matusi, na hata watu kuumizwa au kuuawa kwa tuhuma za wizi. Kuwapiga au kuwaua wezi imeshakuwa kivutio kikubwa mitaani, kama vile burudani. Haya ndio malezi ya watoto wa leo. Watakapokuwa watu wazima, itakuwaje?

Picha hapo juu niliiona kwenye blogu fulani, ila nimesahau. Nitapenda kutafuta chanzo ili niweke taarifa kikamilifu.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli inasikitisha kuona taifa la kesho limeshaanza kuharibika. Ningependa kuwa na sheria za ununuaji wa pmbe na pia Singara kama hapa Swede. Nina maana haya ndio mambo ambayo tunatakiwa kuiga yaani mambo mazuri. Maana utakuta wazazi Afrika hawaona hasara kuwatuma watoto wadogo wakawanunulie bia au sigara.Matokeo yake watoto wengine wanakuwa na hamu ya kuonja kuona kama ni tamu na mwisho wake ni kuanza kunywa na kuvuta mapema. Hapa ni mtazamo wangu tu.

Mbele said...

Dada Yasinta

Marekani ni hivi hivi. Bila kufikia umri fulani, kijana hawezi kuuziwa bia, iwe ni kwenye baa au stoo. Bila kufikia umri fulani, kijana hawezi kuuziwa sigara.

Kwetu Tanzania ni tofauti. Mzazi anakatuma katoto na kikapu cha vyupa vitupu, kaende baa kununua bia na paketi za sigara. Hakuna anayeshtuka.

Haka katoto kanasikia na kuona mengi huko baa, maana walevi wa kwetu hawana dogo :-)

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...